Dizasta Vina - Kanisa - REFIX текст песни

Текст песни Kanisa - REFIX - Dizasta Vina



Kanisa rylics
Yoh!
Salamu kanisa wako mpendwa katika bwana
Katika wana waliotaka kufeli nami nazama
Tangu jana uwepo wako haupingiki
Kisa una nguvu ya kuwavuta wasiosadiki
Sikuhitaji mambo ya kugawana madhehebu
Waumini dhaifu wanahama hama kama wehu
Ikiwa tangu kale wazazi wangu walichanganywa
Basi hakika sitahukumiwa kwa kudanganywa
(Kanisa)
Sidhani ka' upo sawa kunibeza
Maana hata wewe unapitisha dawa za kulevya
Tukianza ku-confess yaliyo nyuma ya pazia
We utachomwa moto alafu mi nitaachwa nakuapia
Sitaki kuamini kuwa sadaka au kusifu kwa fasihi
Ndio vitanipeleka kwa masihi
Kitachonionyesha mbingu ni bidii
Ya kutenda mema so sitaki kujua dini ipi ni sahihi, ah!
Kanisa unatudanganya kirahisi
Nyumba ya mungu ni mioyo yetu nahakiki
Kwakuwa saa hizi
Jua kali njaa hizi zinafanya ukubali kugeuka taasisi
Usinishushe hadhi nikizini
Ikiwa unafuga wachungaji wenye dhambi kama mimi
Kanisa nakupa pole
Nje msafi ndani mchafu naomba tusinyoosheane vidole
Kanisa unaniasa
Niache kutamani vyeo na wewe unajihusisha na siasa
Kama mji wa sodoma ulizikwa na anasa
Mwisho wako upo kama hautabadilika sasa
Haufanani na meli ya nuhu
Unaniomba mchango na kodi nimefeli kumudu
Kanisa unanitapeli kizungu
Unanizungusha haunionyeshi kanisa la kweli la mungu
Eti manabii wana vyeti
Kanisa lina account ya mitandao ya kijamii mpaka benki
Wahubiri wanavutana kinguvu
Kanisa unajitangaza kutafuta umaarufu?
Unapishana na muda hakika
Unachojua pekee we ni kufa kuzika
Unanishauri nije kwako ndoa ikiyumba kanisa
Kichekesho kwamba wewe ndio umeyumba kabisa ah!!
Kanisa nilikuja uniongoze
Nimpende mungu wewe unaifunza nimwogope
Jua kali lilinifunza kukaba nikakupa maisha
Na cha ajabu haujanifunza chochote
Nasikia una pande mbili za sarafu
Upande mzuri na upande unaoingia dili mpaka na wafu
Na unanifundisha baya haliwi na thawabu
Nilikuwa mjinga na sasa nayabashiri majawabu
Tunahitaji mafunzo halisia
Wakati mbinu zako zimejaa mafumbo na sheria
Kanisa tunaishi na wanafki kudadeki
Unajifanya rafiki sababu ya ulafi wa chenchi
Ikiwa huruma ya jah haina kipimo
Basi kati ya wanaoomba msamaha nami nimo
Dhambi zako sawa? Tumezidiana kimo
Mungu aliye hai akuepushie shimo, kanisa huh!
Umeshindwa kukidhi
Utu unakutoka sababu umeshikwa na dhiki
Unasahau lengo unasahau umesimamishwa na sisi
Pesa inakuyumbisha nawe unayumbisha misingi
Kijiwe chako hakikuniingia akilini
Nikafata vijiwe vya pombe vikanitia umasikini
Kisa kila aliyenionyesha nia nilimuamini
Leo siwaoni wote wameingia mitini
Haupo hata kwenye hadhi ya utatu
Mungu baba, mwana, roho kisa kazi za uchafu
Kanisa hauchezi Pasi ni rafu
Unaremba altale kuliko hata nafsi za watu
Kwa sasa ninahisi una bifu
Na taasisi binafsi kwa sababu haukuwa mwangalifu
Kama ndani yako wanaoishi wadanganyifu
Na wanasali hautazalisha watakatifu
Kuwa mkweli ni wapi ulipoishindwa nielewe
Hiyo siri yako hauwezi ukaificha milele
Kama nitachomwa moto wa kukushika ni wewe
Nishakusafisha kuliko kujisafisha mwenyewe aah!!



Авторы: Edger Mwaipeta


Dizasta Vina - THE WONDERBOY MIXTAPE
Альбом THE WONDERBOY MIXTAPE
дата релиза
28-12-2021




Внимание! Не стесняйтесь оставлять отзывы.