Nonini - Genge Love текст песни

Текст песни Genge Love - Nonini



Ehh najua manze jamaa watoto sana sana wamekua waki complain,
Sana sana wanasema yaani
Kenyan men are very unromantic
Nasema pole
On behalf of all the men out there...
Hii ni genge love...
Inaenda kitu ka hii...
(Lady Bee)
Ntakupa jamii, ukinijalii
Nimeapaa...
Uwe msanii, huna ganjii...
Sitakuacha...
Bora unipe unacho naahidi mgenge mi
Nimeapa...
Mapenzi bora yatudumu mi na wee
Bila shaka...
1 (Nonini)
Mtoto kwangu wewe ni ka maua nispokushughulikua ka kukuwekea maji naeza kuua,
Nashkilia roho yako fiti ka glasi nisiiachilie sabu jo, naeza ivunja,
Mtoto wee ni ka thambi au halua,
Na niko sure utamu ya manzi mnaijua,
Nyuma ya kila mwanaume anaendelea kimaisha
Kuna mrembo anamshkilia anam-support kabisa,
Manzi wee ni ka pesa yangu kwa benki,
Nakuhifadhi maisha ya baadaye watoto wengi,
Siunajua wewe ni ka track noma kwa msani,
Feeling yenye wee hunipa nikiwa studio ndani,
Mtoto ni ka hewa ya asubuhi na mapema,
Jua ikikata wingu smile yako unacheka,
Saa hii una-blush unadai nakudanganya,
Ukweli ni ningependa kuomba hizo mbana,
(Lady Bee)
Ntakupa jamii, ukinijalii
Nimeapaa...
Uwe msanii, huna ganjii...
Sitakuacha...
Bora unipe unacho naahidi mgenge mi
Nimeapa...
Mapenzi bora yatudumu mi na wee
Bila shaka...
2 (Nonini)
Mtoto wewe ni ka ndai yangu balaa,
Vile mimi huishughulikia kuiekea tuu hivi ngataa,
Na rangi ya power ndio ikae smattaa,
Shika hii noti kuja tengeza hataa,
Sura nywele shuglikia na vitu kadhaa,
Ndio niringie ma boy wangu vile tu umevaa,
Mtoto najua wewe ni ka paka yangu ya nyumba
Nakupapasa mgongo, nywele na sura,
Matym unaeza kuwa ka simba wa Tsavo,
Najua hutaki manzi mwengine karibu na boy wako,
Cheki vile unatembea ka tausi
Swagger juu na Maringo nafkiria harusi,
Mtoto wewe ni ka pete ile ndakuoa nayo
Itakwama kwa hii mkono wacha rungu ya nyayo
Najua hujazoea kuambiwa vitu ka hizi,
Genge love ndio una-experience sa hizi
(Lady Bee)
Ntakupa jamii, ukinijalii
Nimeapaa...
Uwe msanii, huna ganjii...
Sitakuacha...
Bora unipe unacho naahidi mgenge mi
Nimeapa...
Mapenzi bora yatudumu mi na wee
Bila shaka...
3 (Nonini)
Mtoto wee ni ka gazeti mi huwaga nimekusoma,
Ukinijamia nakuangushia joke moja noma,
Nishakwambia wewe ni ka vumbi ikishakana na mvua,
Inanukiaga aroma moja tu ya ki sure,
Ndio wewe ma cocoa butter ukishajipaka,
Mapua yangu kwa shingo tu najipata,
Mtoto kwangu wewe ni ka kitunguu
Unanitoaga machozi najikausha tu vigumu,
Labda waeza sema jo hii story haikubambi,
Hakuna mahali naenda hapa nadunga kambi,
Jah jah mwenyewe niko sure akikuona yeye hucheka,
Malaika wanamgotea moral! vile alikujenga
Kuna vitu mob sana naeza ku compare nazo,
Lakini hii, hii ndio mwisho ya mawazo,
Wewe ni ka mstari ya mwisho kwa ngoma,
Venye ina-blend fiti na inaingiza chorus ha...
(Lady Bee)
Ntakupa jamii Ukinijalii
Nimeapaa...
Uwe msanii huna ganjii...
Sitakuacha...
Bora unipe unacho naahidi mgenge mi
Nimeapa...
Mapenzi bora yatudumu mi na wee
Bila shaka...



Авторы: Hubert Nakitare


Nonini - The Godfather
Альбом The Godfather
дата релиза
29-07-2014




Внимание! Не стесняйтесь оставлять отзывы.