Mrisho Mpoto - Asanteni Kwa Kuja текст песни

Текст песни Asanteni Kwa Kuja - Mrisho Mpoto



Baba kaja na swali mama kanipa jibu ili niulizwe swali, eeh! swali x2
Asanteni kwa kuja
Ndugu zangu, marafiki zangu
Asanteni kwa kuja
Majirani zangu
Asanteni kwa kujax2
Oyo oyoo
Ndugu zangu, jamaa na marafiki zangu, waneni husema, usimuhadithie mtu ndoto yako ya jana usiku, lakini hapa ni kinyume
Siri tunasema bayana tunaficha
Poleni sana kwa kuja, najua...
Wakati ni mali, wakati ni ukuta
Kama neno litokalo mdomoni
Kama sauti na pengine ni kama moshi ukitoka haurudi lakini kwanini
Dobi kutakasa kaniki ali tunajua rangi ya nguo ndugu zangu ukiona paka kakubali kulala chari anza kuomba ruhusa kazini
Najua, mila na desturi za kwetu huruhusiwi kusema, utaambiwa una gubu una hila uchuro, huna malezi ya pande mbili na kama watakuwa wamechukia sana watasema uliaza kutoka miguu badala ya kichwa
Yaani huna adabu asanteni sana kwa kuja, mimi sikuwa naijuwa safari hii kabla japo niliitegemea sana
Wazazi wangu waliwahi kuniambia
Kuwa ipo siku nitasafiri, nilicheka sana lakini wao walicheka mara mbili, walinitazama kisha wakacheka tena mara ya tatu, tena kwa nguvu, basi kama tofauti ya vicheko vyao nilingelijua usiku wa jana kabla ya leo nadhani ningeudhihirishia uma ule usemi wa kuwa, riziki ni kama ajali, hauitambui siku ya kuja, cha kushangaza baba alishika swali, mama akanipa jibu
Niulizwe swali
Je ungependa kuona nini unapokuwa safarini mwanetu kipezi?
Mama akasema mwambie ungependa kuona miti inavyorudi nyuma wakati wa safari
Ningependa kuona miti inavyorudi nyuma wakati wa safari
Gudi gudi gudi sana kiziwanda wetu
Nini tena kiziwanda wetu?
Mwambie, ungependa ule wakati wa uchimbaji dawa kati kati ya safari
Ningependa ule uchimbaji dawa kati kati ya safari, ha ha ha ha! wao umekuwa kiziwanda wetu
Oy oyoo
Asanteni kwa kuja x4
Haa; ndugu zangu kwa sasa sicheki
Nakumbuka majibu yangu ya kupewa, poleni sana kwa kuja
Nawapa pole wote kwa kufunga maduka yenu kuahirisha shughuli zenu za lazima, kuwadanganya
Waajiri wenu ili tu mnisindikize ndugu yetu, aidha kuogopa lawama mtaani pia labda kujua safari huwa inaazaje, yote ya yote nasema asanteni japo neno hili halina maana tena siku hizi
Nafurahi James kukuona tena huku mbele kama sijakosea kuhesabu umebeba mara sita umempita hata kasim pale nyuma, yeye amebeba mara tano, muda mwingi alikuwa abapiga zogo na kuuliza, tatizo lilikuwa nini mpaka naenda?
Sadiki sikumuona kubeba ila namuona kama hana raha tena mwenye haraka
Wakati naandaliwa aliniuliza peter na Juma huwa inachukua muda gani mpaka safari kumalizika eh! eh!
Oyo oyoo,
Ndungu zangu atupaye tupe humrudia mwenyewe, naomba mpunguze mwendo
Mzee mpiri siwezi kumlaum
Maana umri umepita sasa
Oyo oyoo
Naomba msiende mbio, mtamuacha wakati na yeye ana nia ya dhati, kushuhudia safari ya pili, mh; mh!
Nilikipenda sana kile kikao cha jana cha kuamua leo ndio niende
Kula kunywa, gharama kwangu
Gharama kwangu nitatoa mimi maana nina uchungu kweli! kweli ndio fimbo ya kumkamatia muovu.
Baba kaja na swali mama kanipa jibu ili niulizwe swali, eeh! swali x2
Asanteni,
Ndugu zangu kwa kuja
Marafiki zangu
Asanteni kwa kuja
Majirani zangu,
Asanteni kwa kuja
Oyo oyoo,
Asante kwa kuja x2
Oyo oyoo
Oyoo oyoo
Oyo oyoo
End#########



Авторы: Mrisho Mpoto


Mrisho Mpoto - Waite
Альбом Waite
дата релиза
30-01-2015




Внимание! Не стесняйтесь оставлять отзывы.