Rayvanny - Kwetu Songtexte

Songtexte Kwetu - Rayvanny




Sifa kwa Mola wangu Maulana kwa mengi aliofanya
Hadi mi na we kukutana, kisura
Sijapanga kudanganya, ntasema ukweli mama
Kisa nakupenda sana, kisura
Umesema wanipenda
Ila maisha yangu maseke
Michicha, milenda
Ndo menyu yangu, na ya kuku mateke
Yaani chenga
Kila siku kilio sa lini nicheke?
Sina tenda
Ugali Buguruni, mboga Temeke
Nafurahi umeniridhia niwe na wewe kimwali
Maisha yangu mitihani isoisha maswali
Ukifika nyumbani vumilia maana hali sio swali
Asubuhi mchana pakavu, jioni ndo kula futali
Tena huku kwetu muda wowote mateja wanatinga
Viwalo vyetu ukifua kumbuka kuvilinda
Huku kwetu muda wowote mateja wanatinga
Mwali wee, suala la nyumba na gari mimi
Bado, mi bado (mi bado)
Ndo kwanza nimepanga
Bado, mi bado (iyee)
Sina hata kiwanja
Bado, mi bado (iyee)
Kulipa kodi majanga
Bado, mi bado (mimi bado)
Mtaani kwetu hekaheka ukienda sokoni kariri vichochoro
Ghetto namkeka tu hakuna kitanda, shuka wala godoro
Hekaheka hakuna kibatari ndani giza totoro
Mvua ikinyesha nyumba inageuka ka boti ya Comoro
Ila nimeshakupa, nimeshakupa mtima mtima
Ukija kususa, utanizika mzima mzima
Nimeshakupa eh, nimeshakupa mtima mtima
Ukija kususa ah, utanizika mzima mzima
Tena huku kwetu muda wowote mateja wanatinga
Viwalo vyetu ukifua kumbuka kuvilinda
Huku kwetu muda wowote mateja wanatinga
Mwali wee, suala la nyumba na gari mimi
Bado, mi bado (mi bado)
Ndo kwanza nimepanga
Bado, mi bado (iyee)
Sina hata kiwanja
Bado, mi bado (iyee)
Kulipa kodi majanga
Bado, mi bado (mimi bado)
Suala la nyumba na gari mimi
Bado, mi bado (haki ya Mungu, bado)
Ndo kwanza nimepanga
Bado, mi bado (iyee)
Sina hata kiwanja
Bado, mi bado (iyee)
Kulipa kodi majanga
Bado, mi bado (mimi bado)



Autor(en): Rayvanny



Attention! Feel free to leave feedback.