Darassa - Nishike Mkono Lyrics

Lyrics Nishike Mkono - Darassa



Nobody see me crying
All I know is nobody by my side
Mungu nishike mkono
Nishike mkono (nishike mkono)
Nishike mkono (nishike mkono)
Nishike mkono (nishike mkono mkonoo)
Mwili kama una vidonda ukinigusa tu naumia
Kichwani mizigo ya dhambi gunia kwa magunia
Dunia sinia pakua unachoweza
Nirudishe kwenye njia walimwengu walishanipoteza
Mpaka leo bado mwanangu yupo magereza
Mtoto wa jirani anasomeshwa uingereza
Babaake na Athumani alikufa mvuvi wa pweza
Mwenye utajiri wa imani masikini wa kifedha
Washanichimbia kaburi wanizike nahema
Washakata miti ya vivuli mifereji ya neema
Unaweza kuta unaemuamini ndio anaekuwekea sumu
Hawana alama binadamu anaekuja kukuhukumu
Mwili umechoka naforce tu kuendelea
Mpaka naogopa wapi naenda kutokea
Hata nikiokoka nani ataniletea
Nisipotoka maisha yananitokea damn
Nobody see me crying all I know nobody's by my side Mungu nishike mkono
Nishike mkono (nishike mkono)
Nishike mkono (nishike mkono)
Nishike mkono (nishike mkono mkonoo)
Kumekucha nipo njia panda sioni hata pa kuelekea
Na kiza ndio kinatanda niendako nani wa kunipokea
Nishike mkono (nishike mkono)
Nishike mkono (nishike mkono)
Nishike mkono (nishike mkono mkonooo)
Unajikuta uko peke yako giza kubwa kwenye mtaa
Huoni ndugu wala jamaa uliokuwa nao jana bar
Mawazo ya karaha nafsi inakosa raha
Upepo mkali na baridi bila koti la kuvaa
Unajiuliza Mungu where you are uoneshe njia
Kelele za uchungu na hakuna anaekusikia
Usitamani kiatu changu we ukivaa hautembei
Ikiwa ni siku mbaya ndio masaa hayasogei damn
Nobody see me crying all I know is nobody by my side Mungu nishike mkono
Nishike mkono (nishike mkono)
Nishike mkono (nishike mkono)
Nishike mkono (nishike mkonoooo)
Ayoo imagine maisha ya mtoto bila mzazi wa kumlea
Nambie ndoto za wangapi mitaani zimepotea
Imagine mzazi wa lulu maumivu aliyojibebea
Sometimes tunaishi nje ya malengo tuliyojiwekea
Kifuani kama kuna moto Moyo wangu unaungua
Maumivu nnayopata usitamani kuyajua
Nashindwa kupiga hatua uwoga nasuasua
Maji yakiwa shingoni ndio nakumbukaga dua
Nashindwa kuchagua kati ya mvua na jua
Kuna kitu kinamiss nawaza kukigundua
Natamani kuwa mtoto kibaya haiwezi kuwa
Vazi la dhambi nililovaa halitakati hata nikifua
Mwili umechoka naforce tu kuendelea
Mpaka naogopa wapi naenda kutokea
Hata nikiokoka nani atakaeniletea
Nisipotoka maisha yananitokea
Nobody see me crying all I know is nobody by my side Mungu nishike mkono×2
Nishike mkono (nishike mkono)
Nishike mkono (nishike mkono)
Nishike mkono (nishike mkono)



Writer(s): Darassa


Darassa - Nishike Mkono
Album Nishike Mkono
date of release
24-04-2017




Attention! Feel free to leave feedback.