Lyrics Shahidi - Dizasta Vina
(Reporters
speaking)
Ah
Nilipanda
kwenye
jukwaa,
watu
walinishangaa
Unadhifu
wa
meli
haukufanana
na
nilivyovaa
Kabla
sijatoa
salamu,
walipoteza
hamu
Ya
kuburudika
wengine
wakaanza
kusambaa
Nilikuwa
na
nywele
nyingi
Zilionyesha
pia
siku
ni
nyingi
tangu
mara
ya
mwisho
ziwekwe
maji
Wale
Matajiri
waliosheheni
kwenye
viti
walicheka
wakihisi
Mi'
chizi
au
mchekeshaji
Walio
karibu
pia
wakaanza
kun'tunza
pesa
Na
walio
mbali
walijaribu
kurusha
fedha
Kwa
yote
niliyowaeleza
hakuna
alieyaweka
kichwani
Wote
walihisi
kuwa
nataka
kuchekesha
Walinitemea
shombo
kwa
kejeli
Wengine
walihisi
nalianzisha
zogo
kwenye
meli
Mwonekano
haukuyabeba
maneno
yangu
Hawakuamini
niliposema
kuwa
chombo
kina
mushkeli
Niliwaeleza
kuwa
kule
ndani
kuna
tundu
dogo
Linapitisha
maji
linazamisha
chombo
Waliendelea
kujadili
siasa
na
vibonzo
Hakuna
aliyejadili
kuhusu
roho
Za
wasakatonge
wanyonge
wasafiri
daraja
la
tatu
Hawakulipa
pesa
nyingi
ila
walikuwa
ni
watu
Maji
yalianza
kuingia
vyumbani
mwao
Iliwekwa
mipaka
hivyo
taarifa
hazikufika
katu
Nilienda
mpaka
chumba
cha
sauti
Nitoe
tangazo
kabla
hatujakumbwa
na
mauti
Mtoa
sauti
aliwataja
matajiri
Akiwapa
sifa
majina
makubwa
na
saluti
Niliwaambia
wekeni
glasi
chini
mtege
masikio
Hizo
kelele
mnazosikia
si
sherehe
ni
vilio
Wakasema
nimedata
nataka
kuanzisha
vagi
Ilionyesha
wazi
hawakuona
mbeleni
tishio
Hata
kwenye
vyumba
vya
wasomi
maarufu
Vyeti
walihodhi
maradufu
Niliwahoji
kuhusu
ubovu
wa
meli
wengi
Waliujua
ubovu
lakini
walisema
haiwahusu
Naapa
haki
nilienda
kote
Nilihamaki
kuona
wote
wamepewa
cocktail
Walikunywa
na
kula
bata,
walikunywa
hata
Mziki
waliruka
mpaka
mafundi
walilewa
pombe
Wakasema
huyu
ni
mjinga
hajielewi
Kisha
wakanituhumu
mi'
ni
mlevi
wakati
Wamelewa
wao,
wakanipa
matusi
ya
kienyeji
Hawakutaka
kusikiliza
hata
semi
Nilimwona
nahodha
nikahisi
nimeipata
nafuu
Alikua
kando
ya
mrembo
fulani
hivi
daraja
la
juu
Gauni
refu
mwili
mzima
amepakaza
tatuu
Aliponiona
aliendelea
kuikata
tamboo
Kweli
starehe
inaweza
kukufanya
hauoni
Kukufanya
hauoni
Kwani
licha
ya
kujua
nipo
hapo
kutoa
Taarifa
nahonda
na
mrembo
waliendelea
kushikana
maungoni
Nahodha
akaipaza
miguno,
akinipuuza
Mrembo
naye
akafata
mkumbo
Nahodha
akachukua
chupa
akakata
mafundo
Wakaendelea
kupapasana
mifumo
Ya
viungo
vyao
vya
uzazi
walikuwa
radhi
kuzika
shift
Hawakusikia
chochote
nilichosema
Nakumbuka
mrembo
alidiriki
kuniita
mwizi
Nikafatwa
nikaja
kupigwa
na
walinzi
Wenzangu
waliogundua
ubovu
wa
chombo
walihofu
Wakaamka
wakawahi
kubeba
vyombo
vya
wokovu
Walikaa
kimya
kwa
sababu
tu
ya
ubinafsi
Mi'
nikabaki
ili
niziokoe
roho
za
wachovu
Ilikuwa
bahati
mbaya
hakuna
aliyesadiki
Mshereheshaji
akaongeza
sauti
kubwa
ya
mziki
Kiasi
sauti
yangu
ikaanza
kuwa
haisikiki
Walinzi
walitumwa
wanidhibiti
Nilifungwa
kwenye
chumba
chenye
giza
chini
nisihame
Nikachapwa
mijeledi
thelathini
na
minane
Nikapambana
nikatoroka
na
mtumbwi
kwenda
kando
Usalama
wangu
ulianza
hapo
Nilishuhudia
kila
inchi
ya
ile
meli
ikizama
Roho
za
kila
mkwezi
zikihama
Kutoka
uhai
kwenda
kifo,
sikufurahi
kuona
hivyo
Ila
sikuwa
na
jambo
ningeweza
'fanya
Wakati
walokole
wakiombea
kupona
Tajiri
na
maskini
waligombea
maboya
Wanazi
walionicheka
wakasema
mi'
ni
zuzu
Walikufa
wote
hata
walionisema
kinoma
Ahadi
ya
maisha
mapya
ilisemwa
ila
hakuna
aliyekumbuka
Pesa
zilizagaa
na
hazikuguswa
Hata
wale
waumini
walioitamani
mbingu
Na
kuisifu,
kumbe
wote
waliogopa
kufa
Waliokuwa
wanajikweza
na
ukubwa
na
ubosi
mwingi
Yaliwaishia
majivuni
Njia
walizibuni,
waliua
mpaka
wenza
ili
'kufosi
kingi'
Kifo
kiliwatia
mbavuni
Walikufa
wengi
kama
kuku
kote
walizagaa
Hata
wanajeshi
waliozijua
'kareti'
'Walidedi'
maana
ujuzi
wa
mitutu
haukufaa
Mbele
ya
kufa
hakuna
mwenye
nguvu
au
shujaa
Nilishuhudia
makafiri
wakiungama
Masikini
na
Matajiri
waligusana
Utu
uliwatoka
uasi
ulisogea
Tofauti
za
kabila
na
rangi
zilipotea
Watu
wenye
bendi
na
'tisheti'
zao
za
kijani
Walisahau
kuwa
nao
pia
wapo
ndani
Milango
ilokuwa
wazi
yote
ilijifunga
Walipiga
kelele
na
mwisho
walikufa
maji
Washairi
waswahili
na
tashtiti
zao
Matajiri
na
masikini
wote
chini
yao
Kwaya
hazikutoa
sauti
ndimi
zao
Walikufa
wote
mpaka
mahujaji
na
dini
zao
Wakati
wa
kufa
hakuna
dawa
Hakuna
kiongozi
hakuna
chawa
Hakuna
tofauti
ya
mali
na
milki
zetu
Kwenye
kufa
hata
wenye
nacho
na
wasio
nacho
wanakuwa
sawa
Hazikusaidia
diplomasia
za
digitali
Asili
ilihakikisha
walosalia
hawafiki
mbali
Waliendelea
kungoja
msaada
kwa
tumaini
Mwisho
wote
walikufa
sababu
ya
baridi
kali
Walikufa
makini
sababu
ya
wapuuzi
wachache
Walofanyia
uzembe
tangazo
langu
Wamiliki
walikula
bima
wakasingizia
ajali
Ilihali
meli
ilizama
mbele
ya
macho
yangu...
ah!
Viongozi
hawakubebwa
na
vyeo
vyao
Maana
wote
walikuwa
mbali
na
ridhaa
Niliona
kofia
za
ufalme
zikielea
kando
yao
Ila
hakuna
aliyekuwa
hai
kuzivaa
Niliwapa
taarifa
lakini
wakanitwika
maudhi
Waliishia
kulia
na
hazikusikika
sauti
Walipambana
Mwisho
yaliwafika
mauti
Nilibaki
hai
kuziandika
sarufi
Attention! Feel free to leave feedback.