Ferooz - Wema Wangu Umeniponza Lyrics

Lyrics Wema Wangu Umeniponza - Ferooz

Uuh, uuh
Uuh, uuh
Wema wangu umeniponza, sasa machungu ya Dunia nayaonja
Wema wangu umeniponza, sasa machungu ya Dunia nayaonja
Wema wangu umeniponza, sasa machungu ya Dunia nayaonja
Wema wangu umeniponza, sasa machungu ya Dunia nayaonja
Ni mijeledi ya Bwana Afande, ni mijeledi ya Bwana Afande
Ni mijeledi ya Bwana Afande, ni mijeledi ya Bwana Afande
Pamoja na magonjwa, mwilini yalionielemea
Na ujumbe niliotumiwa, toka kwa yangu familia
Kwamba huko uraiani, wao wanateketea
Ghafla, machozi yakaanza kunidondoka
Mara mfungwa mwenzangu, aliyekuwepo pembeni yangu
Akaniuliza swali, ambalo liliniongeza machungu
Akaniuliza "nini, kinachokuliza
Na, ni mkasa gani, uliokuleta humu kwenye giza"
Mwenzenu mpaka hivi sasa nashindwa kuamini kwamba
Wema wangu, ndio umeniweka mi kizani
Urafiki wetu ulikua kama ndugu tulioshibana, niliamini yeye
Ndiye mwenzangu, wa kufa na kuzikana
Habari zikanifikia kwamba, mwenzangu yupo matatani
Ilibidi niende kumsaidia, kwani mimi ndio rafiki yake maishani
Na ilibidi ahukumiwe, hukumu kubwa sana
Ili kumsaidia ikabidi nimtolee dhamana
Dhamana ikaniponza mimi, ile dhamana ikaniponza mimi
Kwani, ghafla swahiba wangu ye akatokomea
Na haikujulikana wapi alipoelekea
Nikawekwa chini ya ulinzi, niliyemtolea ile dhamana
Nikisubiri uamuzi wa mahakama
Wema wangu umeniponza, sasa machungu ya Dunia nayaonja
Wema wangu umeniponza, sasa machungu ya Dunia nayaonja
Wema wangu umeniponza, sasa machungu ya Dunia nayaonja
Wema wangu umeniponza, sasa machungu ya Dunia nayaonja
Ilipofika siku ya hukumu, mie kwangu nikaiona kama sumu
Nikapelekwa mahakamani, nikapandishwa kizimbani
Bwana Hakimu, na hakutaka kunielewa asilani
Akanihukumu kifungo cha maisha, yaani naweza sema alimaanisha
Kwamba maisha yangu yote, mi nitaishi gerezani
Na sitotoka mpaka nikapotoweka Duniani
Bwana Hakimu, akaigonga nyundo mezani
Mke wangu analia bila matumaini yoyote
Watoto nao wanalia bila kuelewa chochote
Sababu ni wadogo sana, wale watoto ni wadogo sana
Natumikia kifungo cha maisha
Oh, ooh
Oh, ooh
Ah, aah
Ah, aah
Wema wangu umeniponza, sasa machungu ya Dunia nayaonja
Wema wangu umeniponza, sasa machungu ya Dunia nayaonja
Wema wangu umeniponza, sasa machungu ya Dunia nayaonja
Wema wangu umeniponza, sasa machungu ya Dunia nayaonja

Ferooz - Safari
Album Safari
date of release
20-05-2015

Attention! Feel free to leave feedback.