Gloria Muliro - Mapito Lyrics

Lyrics Mapito - Gloria Muliro



Ey yeah
Ey yeah
Hee he he
Mimi nashangaa kumbe wakati wa mapito
Mambo yote hubadilika
Mmmh
Mimi nashangaa kumbe wakati wa mapito hata rafiki anakutoroka
Mimi nashangaa kumbe wakati wa mapito hauna wa kukutia moyo
Jamani
Kweli nashangaa kumbe wakati wa mapito mambo yote hubadilika
Mmh
Hizi miaka zote mpenzi tumekua tu vizuri
Lakini kuanza jana unabadilika
Ooh ooh
Hutaki kuniona kunikaribia hutaki mpenzi
Kosa unasema kwamba sinanga pesa
Hizi miaka zote mpenzi leo ndipo
Umefungika macho umeona kwamba sinanga pesa
Afadhali niache jinsi ulivyo nipata
Najua ni mapito tu Bwana ananishughulikia
Nasema siezi. Kumwacha Mungu wangu. Ju yako penzi.
Mungu wangu ananishughulikia tu Eeh ehh
Uchungu wa Mwana ni mzazi aujuaye
Mapito yangu baba mwenyewe ndio anaona
Jamani wakati wa mapito
Mapito ohh oh
Usingojee kupigiwa makofi bali kupigwa makofi
Jamani wakati wa mapito
Usitarajie kutiwa moyo bali kuvunjwa moyo
Wakati wa mapito. Mapito oh
Usitarajie marafiki bali manafiki kibao
Utakapo pata wengine wao watakurudia
Watasema wanakujua watasema walisimama na wewe
Aah usiwakemee
Mungu Mungu ndiye analipaye
Uchungu wa mwana
Uchungu wa mwana ni mzazi(ni mzazi aujuaye) aujuaye
Mapito yangu(mapito yangu. Machozi yangu) baba mwenyewe anaona
Atatenda tu tenda tu
Yeah eeh eh
Uchungu wa mwana ni mzazi aujuaye
Mapito yangu baba mwenyewe ndio anaona



Writer(s): Gloria Muliro


Gloria Muliro - Msaidizi
Album Msaidizi
date of release
07-05-2018




Attention! Feel free to leave feedback.