Kidum Kibido feat. Lady Jaydee - Nitafanya Lyrics

Lyrics Nitafanya - Lady Jaydee , Kidum Kibido



Tutu turu tutu yeah
Tiru turu tuntu tu
Tuntu tuntu tuntu
Tun tiriri tin tiriri
Ikiwa umeamua kunitoroka
Ikiwa unahisi kwamba hujisikii nami tena
Na mbona imekuwa ngumu kunidokeza?
Naona ni bora nilie leo badala ya kesho
Kupenda usipendwe
Ni kama kujitia kitanzi
Nitachimba na sururu
Kwa ardhi nikitafuta penzi lako
Ni heri nipigwe fimbo kwa mwili
Sababu nitajikuna ama nitajikanda na maji moto
Maumivu ya penzi mtu hajikuni
Wala hajikandi na maji, na hakuna upasuaji
Kama kuna kosa nimewahi fanya (nieleze)
Kama kuna jinsi tunaweza leta (mpatanishi)
Na kama kuna kitendo ningeweza tenda (nieleze)
Nitafanya (fanya)
Nitatenda (tenda)
Nitafanya (fanya)
Nitatenda (tenda)
Nitafanya nasema (fanya)
Nitatenda (tenda)
Nitafanya (fanya)
Nitatenda (tenda)
Kweli hukumbuki uliyoyafanya?
Ni kweli unakumbuka tulipotoka?
Sisemi habari zozote za kusikia
Bali kwa ushahidi niliouona
Msamaha mara ngapi
Umeshaomba na bado?
Je, ni makosa mangapi
Niliyoyafumbia macho?
Mpaka leo nahisi kufika kikomo
Maumivu yanazidi ndani ya moyo
Sitaki kwenda mbali kwani upo moyoni
Nikusamehe mimi mara ngapi we?
Nieleze, mpenzi, mara ngapi?
Unataka nikusamehe mara ngapi? (usihesabu)
Ungependa nikuvumilie mara ngapi? (bila mwisho)
Je, wewe, nikulilie mara ngapi? (vumilia)
Sitoweza (utaweza we)
Nimechoka (usichoke)
Nimeshindwa (usishindwe)
Naondoka (usiondoke mamy)
Sitoweza (tirindi ndindi...)
Nimechoka (mmh mmh mh usichoke)
Nimeshindwa (usishindwe)
Naondoka leo
Ukihesabu ni mara ngapi umenisamehe
Ni kama kuhesabu
Ni mara ngapi mtoto kaharibu nappy
Usichoke, usiondoke, usilie, niko hapa kukulinda
Kama kuna kosa nimewahi fanya (nieleze)
Kama kuna jinsi tunaweza leta (mpatanishi)
Na kama kuna kitendo ningeweza tenda (nieleze)
Nitafanya (fanya)
Nitatenda (tenda)
Ni do do do (fanya)
Nitafanya (tenda)
Nitafanya (fanya)
Nitatenda (tenda)
Nita-do I swear (fanya)
Nitafanya (tenda)
Unataka nikusamehe mara ngapi? (usihesabu)
Ungependa nikuvumilie mara ngapi? (bila mwisho)
Je, wewe, nikulilie mara ngapi? (usilie) (univumilie)
Sitoweza (unaweza)
Nimechoka (usichoke)
Nimeshindwa (usishindwe)
Naondoka (uuh uuh uuh)
Sitoweza (usichoke njoo)
Nimechoka (pimpi parara pimpi)
Nimeshindwa (pampa para rara)
Naondoka leo (para rara pampara)
Usishindwe baby
Nita-do-do-do do-do-do do



Writer(s): Nimbona ''kidum'' Jean-pierre


Kidum Kibido feat. Lady Jaydee - Kidum: Collection, Vol. I
Album Kidum: Collection, Vol. I
date of release
26-02-2017



Attention! Feel free to leave feedback.