Mrisho Mpoto - Nimwage Radhi Lyrics

Lyrics Nimwage Radhi - Mrisho Mpoto



Alilililiiii
Ayo lazier
Furaha isio kifani, kumpata mwandani
Hakika wamependeza, Ngoma lipo uwanjani
Kaibiwa Nani, sa unaachaje kucheza
Hama kweli harusi imefana, Tena ya kihistoria,
Pande zote baba na mama, Naona wanashangilia
Ila sitaki kua mnafki, Jumba bovu kuniangukia
Nina langu la moyoni, ningependa kuwaambia
Bi harusi, mashoga wakupupia, Hao niwakuwaangalia
Wako wale wahali gani, wanakuja kuchungulia
Uwaombe samahani, uwakomeshe wambea
Eti, wifi umepika nini, na mimi utanigaia
Waambie, wamepika p dagaa, zenye pilipili nyingi
Zakutisha we na mumeo, wao watakimbia
Aiiii shemeji ndugu yo mumeo, usisikilize ya fulani
Na hii ndio message Sema na mumeo usifate ya jirani
Kwa Furaha niliyo nayo,
Niacheni nimwage radhi,
MI nataka nimwage radhi.
Ai yoi yooo
Niacheni nimwage radhi
MI nataka nimwage radhi
Alilililiiii
Ng'ombe anapoita ndama, tunasema kua analia
Kupigwa na kulalama, hatujawahi kusikia
Hakika mmependeza
Ninavyomfahamu Biharusi, sipati kusimulia
Nimetoka Ruvuma, Mchomori, namtumbo,
Lindi, mtwara mpaka chitohori nimezisikia
Sifa za binti huyu, Mola amemjalia
Binti hapendi majungu, Hakika ninawaambia
Ukimuazia viatu na gauni,
Anakuachia
Bwana harusi tunakupa mke, ukaishi nae vyema nyumbani
Huna kitu usimfiche mwambie, taabani
Ikiwezekana mkakope, mkono uende kinywani
Usimpige mateke, kisingizio kitu fulani
Ooh
Umefanya nini Jana, hakuliki leo ndani
Mtoto bado mteke, usimkomaze Kwa ngumi
Ukimshindwa mrudishe, kwao hajaua huyu
Mumeo akienda kazini, akirudi salimia
Wala usikae chini, chakula kumsukumia
Bali mkaribishe ndani, Hali kumjulia
Muulize za kazini, Kwa tabasamu muruua
Kisha msindikize bafuni, hata kama anapajua
Halafu wewe tafuta kiti, jikoni kimbilia
Chukua simu yako message, ukimtumia
Mwambie
Hasilani bila wewe, chakula hakitaingia
Eh
Aiiii shemeji ndugu yo mumeo usisikilize ya fulani
Na hii ndio message Sema na mumeo usifate ya jirani
Kwa Furaha niliyo nayo
Niacheni nimwage, radhi
Alilililiiii
MI nataka nimwage, radhi
Niacheni nimwage, radhi
MI nataka nimwage, radhi
Alilililiiii
Naomba niishie hapa, tarishi huwa afungwi
Naomba nichape Lapa, yaliyobaki niyamakungwi
Niliyo wakera samahani, kusema ni jukumu langu
Nawaomba muishi Kwa Amani, hiyo ndiyo Furaha yangu
Mhh
Ndoa ni kama safari, tuombeane duaa
Atuepushe na Shari, saa chini ya juaa
Aa Somo yake mwali, ainuke
Mama yake mwali, ainuke
Baba yake mwali, ainuke
Aje Kati tulicheze Goma
Aah
Kaka yake mwali, ainuke
Dada yake mwali, ainuke
Shangazi yake mwali, ainuke
Aje Kati tulicheze Goma
Niacheni nimwage radhi
MI nataka nimwage radhi
Niacheni nimwage radhi
MI nataka nimwage radhi
Wasafi records



Writer(s): Mrisho Mpoto


Mrisho Mpoto - Nimwage Radhi
Album Nimwage Radhi
date of release
14-05-2018




Attention! Feel free to leave feedback.