Rostam - Parapanda Lyrics

Lyrics Parapanda - Rostam



Its rostam baby,
Wanamiliki visenti, mambo yanabuma mipango haisomeki,
Kuna manabii feki ndo maana kuna kila kitu hakieleweki,
Eh, eh parapanda italia parapanda.
Karibu mzee kingunge kwenye makazi ya milele,
Mimi huku nina mji wangu tayari unaitwa nyerere,
Nimeshtuka kukuona huku nini chanzo cha
Msiba? Ni mipango ya Mungu na nimekumisi swahiba.
Vipi nchi yangu mtawala ni chama gani?
Bado ni ccm ingawa kuna upinzani,
Una maana gani kwa hiyo rais ni nani?
Rais ni John ndo anayeongoza usukani, John malecela? no magufuli,
Ulimuacha ni mbunge wa chato sijui unamkumbuka vizuri?
Ah ngoja kwanza unajua haya mambo haya mi nlidhani alipotoka Mkapa
Angefata Jakaya, jakaya alitawa akaja aka retire,
Aliacha mengi yani mambo ni moto mambo ni fire,
Ah mbona nasikia kama hali haiko
Sawa ni kina nani hawa wanajiita ukawa?
Ni wapinzani waliungana lakini hawakumshinda magu,
Wengine chama walihama na bado wakapata tabu, kakomesha ufisadi,
Kaongeza ukusanyaji,
Hakika wamepata mkombozi atakayewafikisha nchi ya ahadi,
Nlisikia siku hizi bunge halionyeshwi kwenye TV maana hoja za
Viongozi wananchi haziwafikii?
Na mitandao ya kijamii je vipi
Haiwasaidii, kuna dada anaitwa mange please hide my ID
Wanamiliki visenti, mambo yamebuma mipango haisomeki,
Kuna manabii feki ndo maana kuna kila kitu hakieleweki. Eh,
Parapanda italia parapanda
Je vipi kaburi langu tayari walilijengea,
Na vipi kuhusu mke wangu maria wanamtembelea.
Kuhusu kumtembelea hilo toa shaka,
Wanamjali na kumlea tena kwa heshima ya mamlaka.
Na nimemwona shemeji yangu ama kweli mnapendana,
Mmefatana penzi la ukweli kufa na
Kuzikana, vipi makongoro mali zangu anazichunga,
Ah bora wa kwako, mwenzie bize na tunda,
Hivi Julius ulikuwa Simba au Yanga,
Kiukweli nilipenda Yanga ila Simba ni kisanga,
Eh Mwalimu unajua hadi kisanga,
Acha hilo nasikia mengi kibamia hadi kudanga.
Nimemwona Komba huku,
Nyimbo za chama anatunga nani,
Mi nasikia wanaisoma namba sijui kaitunga nani.
Sijakuelewa kwani anayesimamia sanaa ni
Nani, lipo baraza ila wasanii wanaishi uani
Wanamiliki visenti, mambo yamebuma mipango haisomeki,
Kuna manabii feki ndo maana kuna kila kitu
Hakieleweki. Eh, parapanda italia parapanda
Kuhusu muungano bado upo au umechuja,
Mpemba anauza kariakoo na mzaramo ana duka unguja.
Ujinga, maradhi umaskini bado bado maadui nipe
Kaifa, ujinga angalau hao wengine janga la taifa.
Na kuhusu barabara zipo, madaraja, yapo,
Kama ni hivyo ina maana uchumi unapanda.
Mh wanadai mchelea ni mbili ukiwa nazo una
Kiwanda, vyuma vipo still kuna hospital hazina vitanda.
Bado nina maswali mengi vipi mwenendo wa
Katiba, mchakato ulisitishwa inasemekana walimpiga.
Walimpiga nani, na ni kina nani na nini alifanya,
Mwalimu sijui ila ni watu wasiojulikana,
Na waliompiga risasi lissu, ni watu wasiojulikana.
Ni kina nani waliomteka roma, ni watu wasiojulikana,
Na wanaoteka waandishi wa habari, sijui ni watu wasiojulikana.
Wanamiliki visenti, mambo yamebuma mipango haisomeki,
Kuna manabii feki ndo maana kuna kila kitu hakieleweki
Eh, parapanda italia parapanda



Writer(s): Rostam


Rostam - Parapanda
Album Parapanda
date of release
01-08-2018




Attention! Feel free to leave feedback.