Sauti Sol - Nenda Lote Lyrics

Lyrics Nenda Lote - Sauti Sol



Umetuma wazazi wako waje wanielezee
Umetuma wazazi wako waje wanielezee
Hunitaki tena
Na mashoga zako waje waniambie
Na mashoga zako waje waniambie
Ndoa tumeivunja
Siamini kuna time singeishi bila wewe
Mapenzi ya kukata na shoka, eeh
Yashamwagika hayazoleki haya, oh
Basi nenda lote mama
Nenda lote mama
Mpenzi unaenda
Nilikuenzi kinomanoma
Yashamwagika hayazoleki haya, oh
Nenda lote mama
Ukatuma lawyer wako aje anisomee
Ukatuma lawyer wako aje anisomee
Kuwa watoto ulonizalia, eeh
Kuwa watoto ulonizalia, eeh
Sitawaona tena
Siamini kuna time tuliapa hadharani
Kanisani kwa chanda na pete, eeh
Yashamwagika hayazoleki haya, oh
Nenda lote mama
Nenda lote mama
Mpenzi unaenda
Nilikuenzi kinomanoma
Yashamwagika hayazoleki haya, oh
Nenda lote mama
Ukatuma pastor wako aje anikemee
Ukatuma pastor wako aje anikemee, mama
Na madeni zangu ukazitangaza, eeh (Ukazitangaza, eeh)
Na madeni zangu ukazitangaza, eeh
Mitandaoni
Shemeji zangu ndugu zako tukionana
Waambie sisi bado rafiki, eeh
Wasinipite barabarani, mama, oh
Umeenda lote mama
Umeenda lote mama
Mpenzi unaenda
Nilikuenzi kinomanoma
Yashamwagika hayazoleki haya, oh
Basi nenda lote mama
Nenda lote mama
Mpenzi unaenda
Nilikuenzi kinomanoma
Yashamwagika hayazoleki haya, oh
Nenda lote mama
Nenda lote mama



Writer(s): Bien-aime Baraza


Sauti Sol - Midnight Train
Album Midnight Train
date of release
10-06-2020




Attention! Feel free to leave feedback.