Lady Jaydee feat. Kidum - Nitafanya текст песни

Текст песни Nitafanya - Lady Jaydee feat. Kidum



Ikiwa umeamua kunitoroka
Ikiwa unahisi kwamba hujisikii nami tena
Na mbona imekuwa ngumu kunidokeza
Naona ni bora nilie leo badala ya kesho
Kupenda usipendwe
Ni kama kujitia kitanzi
Nitachimba na sururu
Kwa ardhi nikitafuta penzi lako
Ni heri nipigwe fimbo kwa mwili
Sababu nitajikuna ama najikanda na maji moto
Maumivu ya penzi, mtu hajikuni
Wala hajikandi na maji
Na hakuna upasuaji oh
Kama kuna kosa nimewahi fanya.nieleze
Kama kuna jinsi tunaweza leta upatanishi
Na kama kuna kitendo ningeweza tenda, nieleze
(Nitafanya (fanya) Nitatenda (tenda)×4)
Kweli hukumbuki uliyoyafanya
Ni kweli unakumbuka tulipotoka
Sisemi habari zozote za kusikia
Bali kwa ushahidi niliouona
Msamaha mara ngapi umeshaomba na bado
Je ni makosa mangapi, niliyoyafumbia macho
Mpaka leo nahisi kufika kikomo
Maumivu yanazidi ndani ya moyo
Sitaki kwenda mbali kwani upo moyoni
Nikusamehe mimi mara ngapi we
Nieleze, mpenzi mara ngapi?
Unataka nikusamehe mara ngapi (unisamehe)
Ungependa nikuvumilie mara ngapi(ningependa univumilie)
Je wewe, nikulilie mara ngapi?
Sitoweza(utaweza we) Nimechoka(Usichoke) Nimeshindwa (Usishindwe) Naondoka leooo
Ukihesabu ni mara ngapi umenisamehe ni kama kuhesabu ni mara ngapi mtoto kaharibu nepi
Usichoke, usiondoke, usilie niko hapa kukulinda
Kama kuna kosa nimewahi fanya, nieleze
Na kama kuna jinsi tunaweza leta, upatanishi
Na kama kuna kitendo ningeweza tenda
Nitafanya.nitatenda...
Unataka nikusamehe mara ngapi
Ungependa nikuvumilie mara ngapi
Je wewe nikulilie mara ngapi
Sitoweza.nimeshindwa... nimechoka.naondoka leoo



Авторы: Nimbona ''kidum'' Jean-pierre


Lady Jaydee feat. Kidum - Ya 5. The Best of Lady Jaydee
Альбом Ya 5. The Best of Lady Jaydee
дата релиза
09-03-2012



Внимание! Не стесняйтесь оставлять отзывы.