Rayvanny - Corona текст песни

Текст песни Corona - Rayvanny



Corona, corona, corona
Nooh ooh olo lo lolo ooh
Mmh hey yy eeh (Mocco)
Wote tumuombe Mungu kwa hili janga
Ikibidi lipite
Tujihadhari na tujikinge
Ili lisitufike
Habari kote duniani zimesambaa
Ugonjwa unaua na hauna tiba
Na wengine wetu masikini hatujiwezi
Mwenyezi Mungu kawe tiba
Watoto wetu mashule, aah
Mama zetu tu sokoni
Kwenye vyombo vya usafiri makazini
Tujilinde
Osha mikono, aaah
Epuka mikusanyiko sio ya lazima, aaah
Na uonapo dalili
Mapema wahi hospitali
Corona, corona, corona
Corona, corona, corona
Corona, corona, corona
Corona, corona, corona
Tanzania hatuwezi tukajiweka pembeni bila kuchukua hatua
′Hatua zimeshaanza kuchukuliwa
Waziri wa wizara ya afya ameshazungumza
Ameshatoa tahadhari mbalimbali
Ambazo tunatakiwa kuzichukua
Napenda nirudie ndugu zangu Watanzania
Kwamba ni vizuri sana tukaendelea
Kuchukua tahadhari, kwa nguvu zote
Ugonjwa huu unaua, na unaua kwa haraka sana
Niwaombe ndugu zangu Watanzania
Tusipuuze ungonjwa huu (Corona, corona, corona)
Tusipuuze hata kidogo (Corona, corona, corona)
Ni lazima tuanze kuchukua hatua (Corona, corona, corona)
Za kujikinga kwa tatizo hili (Corona, corona, corona)



Авторы: Raymond Mwakyusa


Rayvanny - Corona
Альбом Corona
дата релиза
16-03-2020

1 Corona




Внимание! Не стесняйтесь оставлять отзывы.