Dizasta Vina - Fallen Angel текст песни

Текст песни Fallen Angel - Dizasta Vina



Yoh
Wanasema nilipenda bila tija
Kwamba sikutaka kujifunza sikutaka tiba
Nilikupenda na mtaani ilikuwa shida
Nilikosana na watu maana nilikutaja kila mida
Niligombana na wana uliposema nipunguze marafiki
Ulihisi wengi wao wanafiki
Ukasema niache muziki
Nikaacha nikatafuta kazi ilimradi nipambane na dhiki
Nikaona shega
Kama kuna boya yeyote atanilaumu, yamkini bado hajapenda
Niliitika uliponita
Nilifika nikakusikiliza na kila uliponituma nilikwenda
Kama kupenda ilikuwa ajabu
Nadhani hata ile kukonda ilikuwa sababu
Ilikuwa kufanya maamuzi si jasiri
Ila kwa sababu yako wala sikujiuliza mara mbili
Kisa wewe, nikabuni kila mishe
Nikapigana mpaka na kikundi ili nikuridhishe
Nilikuwa mwoga nielewe
Ila nilijipa moyo kuwa chochote kinawezekana kisa wewe
Niliamua nikupende bila doubt
Nilisimama kila nilipoulizwa nika-shout
Sikuogopa ugonjwa wala mauti
Kwa sababu yako, nikakamatwa boda kule Sauzi
Nikukumbushe, shule nilikuwa King kwenye dorm fights
Ila nikapigwa na jamaa kwenye prom fight
Mahusiano yetu yalini-cost
Kuna kipindi nilikosa dili nikazama mgodi
Naumwa mama, hizi shida zipo
Mama yako alipata ajali, nikatoa figo
Nilikuwa nina mafua nakakuhitaji kama chafya ili nitoe
Nilikupenda mpaka ukanigharimu afya
Ulijua kuwa ninapenda Hip Hop lakini ikabidi nijue reggae
Sikuwa tozi lakini nikajua chepe
Nikazijua tembe kichwa kilipokuuma
Nikazama kutafuta ni mapenzi na sikuwa bwege
Nilijitosa kuwa usafiri, nikufikishe
Niliamua kuwa hata mwizi, nikuridhishe
Kaka zako walipanga dili ili waniue
Wakaishia kuniumiza nikakanda mwili
Nilikupenda peke yako, sikujua mingo
Kuna kipindi uliniweka kwenye matatizo
Kwenye vikoba ulikopa hela
Mpaka nikakamatwa mimi nikafungwa jela mwaka
Sikusoma, na sio kwamba nilitaka kufa na mali
Ni kwamba sikutaka uteseke ndio maana nikakupa nyumba na gari
Dili zikabuma na tarehe za kulipa zikatimia
Wadeni walipokuja, nilikimbia
Nilipambana sana bado nikakosa dili
Nikasafiri nikaenda kwa mganga ili niwe tajiri
Sikupenda mwenzangu ufuturu njugu
Nikavuka ukuta mpaka nikaanza kumkufuru Mungu
Ndugu walinikimbia, nakili
Nadhani walihisi zimenikimbia akili
Walidhani ilikuwa simple kuniasa
Walifikia kusema nakupenda wewe kuliko mother
Dah! Nikavunja miiko
Mpaka nikabadili dini nikawa Mkristo
Nilihadaa kufa, tulikosa mboga nikagaa gaa na upwa
Ulipenda kupendeza
Kugeza mitindo ulipenda kuongea kiingereza
Nikakulipia shule, ulifanya madudu
Nikakubali ili usome mimi nibaki mbumbumbu
Nilipigana kila shari ilipokuja
Nilizuga mi ni mwalimu kwa baba'ako
Nilifulia wakaniita McMugga, na mtaani nikawa adimu kwa ajili yako
Nilitaka uwe mke, ni habari
Nilitamani nikupeleke nje ya sayari
Kuna muda nilisanda nikazama kila chaka, sikuogopa Nge ni hatari
Kwa yangu hiyari nikawa pusha
Nilijifanya dalali nikauza gari na nyumba
Mentali, sikungoja zali kunikuta
Mali ulipofuja zote nikaenda mbali kutafuta
Ulitamani rasta, nikasuka
Ulitamani shamba na duka
Ulitamani khanga nikakupa
Sikuogopa nilikudaka ulipoanguka
Washikaji walisema naoa lawama
Nilifunga vioo tukafunga ndoa ya gharama
Kazini nikabeba pesa kwakuwa nilikuwa cashier
Nikakata tiketi twende honeymoon Philadelphia
Sikukwambia haya yote tangu mwanzo
Kwa kuwa sikupenda uteseke kwa mawazo
Nilikulea ka baba'ako, sio mimi yalikuwa ni mapenzi juu yako
Nilishiriki magendo, mpaka kuua
Nilitaka kuwa mjeda nikashiriki depo
Nilitamani kukuoa
Kiukweli ndio maana muda wote huo hatukushiriki tendo
Sikuibuka kilingeni
Nikafunga decoder na subwoofer sebuleni
Kuna kipindi nilikumbwa na madeni ili upate saluni
Nikajenga nyumba ufukweni
Nitapunguza vipi machungu?
Nilikosa nini kwa Mungu
Umekufa sikuoni tena getoni
Umeniacha, Mola akulaze pema peponi
Amen



Авторы: Edger Vicent Mwaipeta


Dizasta Vina - Jesusta
Альбом Jesusta
дата релиза
15-07-2021




Внимание! Не стесняйтесь оставлять отзывы.