Dizasta Vina - The Lost One текст песни

Текст песни The Lost One - Dizasta Vina



Alivaa sketi inayoangaza ilikuwa nyepesi
Fupi unaweza dhani ni kidenti
Japo nilikuwa single ila sikuwa mingle
Alizidisha maringo alipogundua namcheki
Haiba ya aibu mfumo wa kibinti
Kidogo rangi na lile umbo la kimisi
Akiweka pozi nihakiki
Alikuwa anang'aa ila ngozi yake ilisanifu dhiki
Bado ilikuwa hainiboi kumtazama
Macho yangu yalikuwa yana-enjoy alichofanya
Kiasili nilikuwa hoi kiasi cha kutogundua alikuwa na konvoi la mimama
Kwa mtindo wa kujongea kwa madaha
Yule malaika akaanza kusogea nilipokaa
Hata kabla sijaamua kumchunguza
Macho yaligundua kuwa binti anajiuza
Hiyo iliweka ufa moyoni
Nilitamani hata kustuka ndotoni
Kwakuwa nilipata hisia kali za upendo
Nikawa tayari hata kujitupa motoni
Nilitekwa i only needed her for the rescue
That's how far love can take you
Nikataka mpaka kumvika pete
Awe mchumba nikasahau mwenzangu anawaza cash tu
Ni aina ya wasichana wanaotokea kwenye ndoto
Yaani unafumba macho alafu unaona anakulelea watoto
Kwa mara ya kwanza maishani mwangu niliwaza ndoa
Hasa baada ya mapenzi ya wasichana wa town kuniboa
Akiongozana na kundi la wenzake
Akasogea akitoa sauti za kipambe
Kila mmoja akijinadi kwa mikogo ya mahaba
Nakumbuka mmoja alivua brauzi nimtomase
Alijinadi kama ng'ombe mnadani
Nikataka nijitose chakani
Yaani nijitoe sadaka nilimwona kama kidani cha dhahabu
Maisha ya mjini yalifanya ajione hana thamani
Tukagonganisha macho kihisia
Ndio nikajua nimezama na sijui nitakapoishia
Apendae kipofu nikazisahau kasoro
Nikashuka nikamfungulia mlango akaingia
Kwa pupa nikadrive mpaka home
Nilipofika hata kuzima gari sikukumbuka
Kuna muda nilimkuta uchi kitandani
Anauliza kama tunaenda kavu au kwa ndom
Nikamsihi avae nguo
Akahamaki akauliza maswali mawili kwa mkupuo
Jogoo hawiki braza au ume-mix machaguo
Nikamjibu mi msafiri na wewe binti ndio kituo
Kwa jicho la kufuga kisasi
Akanicheki kiasi kwamba niliyumba kinafsi
Akanikumbusha hajaja kwangu kutafuta hifadhi
Anafanya biashara na kwangu amekuja kikazi
Nikashika usemi uchafu ukiingia kwenye kapu toa
Usitupe kapu kwahiyo sikumwona kama changudoa
Nikamwambia nikimwangalia
Kwanza nawaza kujenga pili familia na tatu ndoa
Hakuitikia akanitenga na himaya ya majibu
Moyo wake haufunguki na ninahitaji rai
Hatukuwa sawa nilitaka kujaribu
Akanijibu Kipepeo na nyuki hawatagi yai
Akaniruhusu kumkumbatia
Akashika mikono yangu akaibusu kwa hisia
Sijui alinipa nini nilijikuta naanguka
Kizunguzungu ile kustuka kumekucha
Niliamka na mawenge kichwani
Nilighafirika kugundua hakwepo chumbani
Aliondoka aliniacha na aibu mtaani
Maana aliposepa alibeba kila kitu ndani
Alikuwa kunguru na nilisahau hafugiki
Hata iwe kibudu kwa nyanya na limao haungiki
Alibeba vipi sijui kinachoniuma
Ni kukosa pendo la huyu binti
Sitasahau macho yake mawili ya kirembo
Sauti iliyowasilisha upendo
Akipigwa vikali na ubatili wa matendo
Ya mwili wake mzuri ambao haustahili mateso
Aliniachia meseji alipoondoka
Akinipa pongezi kwamba sikuwa mwoga
Kuufuata moyo wangu akaniomba msamaha
Akisema hawezi kuenzi penzi ambalo kwa wazazi alikosa
Sawa ah! Nimekusamehe zamani mami
Pendo lako dawa ewe baniani
Niahidi utawasamehe wazazi wako pia
Ambao wamefanya uonekane shetani honey
I'm kinda lost I do things i ain't suppose to
I thought you'll be my best friend that I can talk to
I wanna change if you wanna change I'll support you
I think we both need the way out that we can walk through
Ah popote ulipo ambapo info inafika
Bado mrume nipo miaka inapita nauandika
Huu wimbo umenifundisha nisitue mzigo kama ninahisi sijafika
Naoa kesho na nina hamu kukukuta
Nikwambie dunia safi binadamu ndio uchafuka
Ni kawaida usisahau kutabasamu kukikucha
Nakuombea afya kwenye nyama damu na mifupa



Авторы: Edger Vicent Mwaipeta


Dizasta Vina - Jesusta
Альбом Jesusta
дата релиза
15-07-2021




Внимание! Не стесняйтесь оставлять отзывы.