Diamond - Gongolamboto paroles de chanson

paroles de chanson Gongolamboto - Diamond



Poleni wale usiku hatujalala
Wale mabomu yamewapa madhara
Yalosababisha maafa viro hasara
Poleni sana ndugu zangu
Mpaka sasa hawana pakulala
Watoto bado njaa hawajala
Tuzidishe uda na maombi nyingi sala
Poleni sana ndugu zangu
Repeat 2x
Eh mola ona wanao tunakwenda
Eh tunakwenda tunakwenda tunakwenda tunakwenda
Kila siku matatizo bab tushike mikono
Walosema idadi ya watu kadhaa eti wengine majerahaa
Ona wegine wamejifungua maskini mmoja bado
Shida za maisha si usiku si mchana na majanga yanazidi twandama
Huku majukumu yame, Tanzania oh mama ahhh
Kuhusu maidha si usinu si mchana na majanga yanazidi twandama
Huku majukumu yame, Tanzania oh mama eyeeeee
Poleni wale usiku hatujalala (hatujalala)
Wale mabomu yamewapa madhara (mmh madhara)
Yalosababisha maafa vifo hasara
Poleni sana ndugu zangu (eh, Gongo la mboto)
Mpaka sasa hawana pakulala (oh pakulala)
Watoto bado njaa hawajala (hawajala)
Tuzidishe uda na maombi nyingi sala (nyingi sala)
Poleni sana ndugu zangu
Enyi waTanzania wazalendo wa nchii hii
Akuambiaye usikombe mboga siku zote anataka ushibe
Nani anasema usiku mmoja hauozeshi nyama
Huyo tumegeukie na kumtazame mara mbili maana ametudanganya
Pole nchi yangu, pole Tanzania, poleni sana Gongo La Mboto
Ingekua hadithi ningesema ′paukwa', nikaanza kuwaongopea
Ningekua mwana siasa ningesimama jukwaani nakuwaambia nichagueni mimi
Lakini hizi ni roho za watu haya ni maisha
Poleni sana Gongo La Mboto ndugu zangu waTanzania
Apasuaye nguo lazima awe fundi wa kushona
Kilichotokea Mbagala siku ile, watu walizani cinema kule mikoani
Lakini kule Gongo La Mboto,
Hakuna aliyekumbuka viatu wala kumshika mwanae
Hakuna aliyekumbuka mume wala kumbusu mkewe
Najua Tanzania tunavuma kwa ukarimu na upole japokua ni masikini
Lakini uisikia ′puumuuu' ujue kimeshatokew Gongo La Mboto
Tudhihirishe ukarimu wetu na kuitolea Gongo La Mboto
Mungu ibariki Tanzania, mungu ibariki Gongo La Mboto (ibariki)
Eyeeeee
Poleni wale usiku hatujalala (hatujalala)
Wale mabomu yamewapa madhara (madhara)
Yalosababisha maafa vifo hasara
Poleni sana ndugu zangu (ndugu zangu)
Mpaka sasa hawana pakulala (pakulala)
Watoto bado njaa hawajala (ohh hawajala)
Tuzidishe uda na maombi nyingi sala
Poleni sana ndugu zangu




Diamond - Lala Salama
Album Lala Salama
date de sortie
05-02-2012




Attention! N'hésitez pas à laisser des commentaires.