Aslay feat. Khadija Kopa - Usinitie Doa Feat Khadija Kopa Lyrics

Lyrics Usinitie Doa Feat Khadija Kopa - Khadija Kopa , Aslay



Eeh mama tarumbeta
Mwari anamelemeta yeoo ooh ooh
Sifa ninazopata eeeh
Aslay naozesha leo ooh
(Baba harusi hongeraaa)
Ndoa ni jambo kubwa mwanangu
Kaitunze heshima yangu
Chozi linanitoka mwanangu
(Pole we eeh)
Siamini macho yangu
(Ndo hivyo)
Eeeh babu harusi mshike taratibu
Usije ukafuta piko
Haraka ya nini wakati huyo ni mali yako
Mwanangu uchechemee
Ulofundwa usisemeee kwa watu
(Usungo huo)
Maneno umungunye
Ya chumbani usiwape faida watuu mwanangu
Ndoaa usitie doa(mwanangu mwanangu)
Ukitia doa ndoa utanitia haya
Ndoaa usitie doa
Ukitia doa ndoa utanitia haya mwanangu
Wanawake wa kisasa
Mnajifanya mna whatsapp
Hamna muda wa kushughurikia
Waume zenu mtashaha
Mkifanya mchezo wenzio watawasapombe
Ooooh oooh
Usipende kugombana na mume wakoo
Hata kama kuna vitu vimekukwaza
Mwanamke busara
Rudi vikizidi vituko
(Hakukutoa juu ya mti babu eh)
Hapa ni nyumbani kwako hujafukuzwa
Eh Mashoga wataharibu ndoa yako
Watakupindua watamteka mume wako
Jitahidi kuwaheshimu wakwe zako
Hizo ndizo nguzo
Za kuitunza ndoa yako
Wivu usiuendekeze utakutoa roho
Lakini usiwe kama zeze
Kwenye ndoa yako
We jitahidi upendeze uwarushe sana roho
Ila mbali usicheze na mume wako
Ndoaa usitie doa
Ukitia doa ndoa utanitia haya
Ndoaa usitie doa
Ukitia doa ndoa utanitia haya mwanangu
Mwanangu seketua seketua seketu
Baba seketua seketua seketu
Majirani seketua seketua seketu
Wahuni seketua seketua seketu
Nasema babu harusi mmemuona
Babu harusi eeh mmemuona
Babu harusi eeh mmemuona
Aah Bibi harusi eeeh mmemuona
Oho Bibi harusi wohoo wowooh mmemuona
Eeh baba ya mwari eeh mmeniona
Mhh mama ya mwari eeh mmemuona
(Mwanaume harogwi eeeh)
(Anarogwa kwa mambo mambo mambo)
Aslay na hangaika eei eei nisaidie wanangu
Ooh na hangaika eieeh eihh nisaidie wanangu
Babu harusi kahangaike eeieh usaidie wanao
Kaangaike eeieh usaidie wanao
Bibi harusi kahangaike eiee eeh usaidie wanao
Kahangaike eeieh eieeh usaidie wanao




Aslay feat. Khadija Kopa - Usinitie Doa Feat Khadija Kopa
Album Usinitie Doa Feat Khadija Kopa
date of release
15-10-2017



Attention! Feel free to leave feedback.