Dizasta Vina - Nyumba Ndogo Lyrics

Lyrics Nyumba Ndogo - Dizasta Vina



Yeah yeah... innocent mujwahuki.dizasta
Yeah yoh skiza Nyumba ndogo, leo nna ajenda
Naona umenogewa kula mpunga wa mwenza
Unajitapa na mimi ndo nlokuweka
Nashangaa sana nashindwa bomoa nilichojenga
Japo nimekujenga bila msingi madhubuti
Nikiwa kwako huwa nyumba kubwa sikumbuki
Natumikia kifungo
Umenifunga kwakuwa timu yako inajua kutumia viungo
Nimejaribu kutamba bila wewe
Tatizo nkizipata huwa nakufata mwenyewe
Sio kwamba nyumba
Kubwa hainiwezi kunifikisha
Ukweli kwamba utundu wako umeuzidisha
We sio mnyama lakini ninakufuga
Ka unajua siwezi kukuacha bei shusha
Maana hauvumi lakini umo
Nyumba ndogo nzuri tatizo inajengwa nje ya mifumo
Najiuliza nitakwacha lini aisee
Mshahara wenyewe mdogo sa kwa nini tushee
Kwakuwa unapika kile ninachonunua mimi
Nyumba ndogo naomba unambie utakua lini?
Ah yoh mtaani umeshakuwa habari
Hautaki kuolewa hautaki kuijua mahali
Tambua kuwa unaniletea jua kali
Niliwahi kukuchunia mwezi nikanunua gari
Nyumba ndogo nina watoto nina mke na nna madha
Cha ajabu nikipata mtonyo tu nakuwaza
Raha tunapata ila natoa changu
Na unapokea bila ya huruma na ndoa yangu
Unanivua koti unanipa maji
Unanipa majina ya kifalme unanipa hadhi
Unanipa masaji unanipa kazi
Ambayo hata nyumba kubwa huwa hainipagi
Kuta 4 sita kwa sita unajipinda
Sikuzoei kila nikija mitindo mipya
Mingine ya kitanga na kichina
Nalia kama mtoto mpaka nashindwa kutaja jina
Kama ni dawa hii limbwata digitali
Nikiwa nawe huwa nawaza sifiki mbali
Kwakuwa sihudumii nyumba kubwa inanyufa
Ndo maana nyumba ndogo ni imara kuliko kubwa
Yeah sipendi unavyoniita dia au laazizi
Ungenipenda usingenibana hadi saa hizi
Utabaki nyumba ndogo kuwa mke huna hadhi
Nguo kwenye maji nkutofautishaje na mtekaji
Sawa mi nawe wote dunga dunga
We ni spy unajuaje madhaifu ya nyumba kubwa
Unataka utawale una wazimu nadhani
Kivipi uite nyumba kubwa simu ya mezani
Nilijenga nyumba kubwa kwa wenge mwenzako
Sasa kwa usitulie nawe ujenge ya kwako
Kama wewe pia ni nyumba na unajengwa kiuhakika
Jiulize kwanini unajengwa kwa kufichwa
Nyumba ndogo huu ni walaka kwako
Nimechoka kuwa chini ya mamlaka yako
Sipendi nakataa kuwa wakala wako
Natangaza mwisho wa utawala wa zama zako
Nayakosa majukumu
Kama baba,nyumba ndogo kuingia rahisi kutoka ngumu
Nilikujenga nakwenda kukubomoa
Kwa sasa nahitaji kuijenga ndoa
Asanteh



Writer(s): Edger Mwaipeta


Dizasta Vina - THE WONDERBOY MIXTAPE
Album THE WONDERBOY MIXTAPE
date of release
28-12-2021




Attention! Feel free to leave feedback.