Zuchu - Hasara Lyrics

Lyrics Hasara - Zuchu



Ahaaa ahaaa
Mmmh mmmh
(Mr LG)... haaa...
Mi staki tuongee
Moyoni nina machungu machungu
Sije tenda dhambi mmh
Ila chozi la mnyonge
Malipo ni kwa Mungu kwa Mungu
Bora nihame kambi mmmh
Kama subira ina mwisho
Ina mwisho wake maana
Asali umeimaliza mzinga
Ukanifanya tahira
Suluhisho nimeona kwako hamna
Moyo wangu si wa mninga
Najitoa
Tunangombana kwa vitu vidogo
Kosa si kosa unageuka mbogo
Huna dogo wewe
Hunipendi unang′onga kisogo
Punda siendi eti bila magongo
Mpenda zogo wewe
Kukupenda tena staki!
Nimekoma staki!
Kukuona staki!
Narudia tena staki!
Kukuona staki!
Nimekoma staki!
Bora nihesabu
Kwa penzi nimepata
Hasara aah (oh hasara)
Hasara aah
Hasara, hasara
Hasara ya roho
Penzi imekwenda zake
Hasara aah (hasara ni)
Hasara aah (hasara ni)
Hasara, hasara
Kina cha maji matitu
Kanacha bila boya nijifie
Kosa langu nini?
Mchana nauona ka usiku
Nachacha nyie maumivu niyasikie
Yasiwakuteni iiih
Na kama albadiri
Ya bayana umeniumbua
Umeniadhiri
Umeniacha mnyama na nguo umenivua
Kukupenda tena staki!
Nimekoma staki!
Kukuona staki!
Narudia tena staki!
Kukuona staki!
Nimekoma staki!
Heee! Bora nihesabu tu
Kama nimepata
Hasara aah (oh hasara)
Hasara aah (hii hasara)
Hasara, hasara
Hasara ya roho
Penzi imekwenda zake
Hasara aah (hasara ni)
Hasara aah (hasara ni)
Hasara, hasara
(Ka mix Lizer)
Haa, haa, haa...
Bora mi nibaki nalia
Haa, haa, haa...
No no nono noo
Mmmh



Writer(s): Zuhura Soud


Zuchu - Hasara - Single
Album Hasara - Single
date of release
22-11-2020

1 Hasara




Attention! Feel free to leave feedback.