Diamond Platnumz - Mapenzi Basi paroles de chanson

paroles de chanson Mapenzi Basi - Diamond Platnumz



Yalinifanya nikaugua
Mara napanga napangua
Mwili ukakonda nikapungua
Oh sikulala, sikulala
Oh maradhi nikaugua oh
Yakanichoma na kuungua roho
Kutwa nawaza na kuwazua
Sikulala, sikulala
Hayo mapenzi bwana
Hayana maana
Yalinifanya mi nichekwe
Sababu yake nishagombana
Nikatukanwa
Lakini akanipiga teke, ai
Haya mapenzi bwana
Hayana maana
Yalinifanya mi nichekwe
Sababu yake nikagombana
Usiku mchana
Yeye
Mi mwenzenu tena basi
Oh mapenzi sitaki
Oh mwenzenu tena basi
Basi, basi sitaki (mara 2)
Oh nilishagombana na mama mzazi
Akataka nimwagia radhi
Sababu yule fulani
Wa moyo wangu
Yakaleta zengwe kwa kazi
Ugomvi wa simba na panzi
Vurugu kwa majirani
Ai eh Mola wangu



Writer(s): diamond platnumz


Diamond Platnumz - Mapenzi Basi
Album Mapenzi Basi
date de sortie
12-12-2012




Attention! N'hésitez pas à laisser des commentaires.