Fid Q feat. Barakah The Prince - Mafanikio paroles de chanson

paroles de chanson Mafanikio - Fid Q , Barakah The Prince



Kujisikia nipo juu mie sitaki hizo deals
Sipendi makuu hivyo nitabaki kuwa real
Na kila track ya Q aaah,. Ni wazi utaifeel
Ni wazi iko full aah mzazi ninakill
Ninamwagika kama Masika.
Ninaheshimika na sio kanjibai
Kwa huu mziki wa bajaji
Hadi kwa washkaji wenye macadillac
Unawashika ile kibabylon
Unauzika sana maghetoni
Ilimradi tu wawe happy more
Midadi tu ila party no
Mkisinzia mtaniudhi nishawapa vyeo
Tuwape wapuuzi waliodai hii haiuzi haya matokeo
Safari ni hatua, kufika inabidi uianze
Haina kukita au kusita, inabidi ukaze
Ingia, ongoza au fuata njia, kukimbia ni mwiko
Kuanzia ulipo sio sawa na kubakia ulipo
Nikisema 'chini hapana' nina maana fanya unyanyuke
Na ukiamini umesimama mwana. Komaa usianguke
Ukijituma na neema inakaribia
Nyuma walio-give up mapema wangekaza wangeifikia
Penye... Happy, jitusu, unafki usiuruhusu
Yajue ya kuzingatia ili uachane na yasiyokuhusu
Kibongobongo longolongo shazi
Endelea kusaka mchongo hata ukipata kazi
Tunachukiana? Ndio.
Ila sio sababu kuacha riadha ya mafanikio
Ongeza mbio
Sababu kila mtu, kila kona anasaka mafanikio
Haukungoji wakati. Ooh wewe
Zinapita nyakati.ooh wewe
Muda wako bahati. Oh wewe
Na kughairisha kisa haupati sapoti
Ni kujificha na kuuliza giza
Iko wapi ile tochi?
Haupati ile noti
Na wakati wa ule uboss ushapotea
Hautaki ukose? usiache ofcoz endelea
Utafanikiwa kwa unachojua au unachofanya
Wachache ndio hutusua kwa jinsi tu wanavyoonekana
Mafanikio hayaji ukikata tamaa
Yenyewe huwafuata wanaojituma
Na wale wasiosukumwa na njaa
Sipigi kila dili mipaka imezingatiwa
Sitaki kuwa tajiri ninataka kufanikiwa
Ili kuheshimiwa kwanza ni lazima ujiheshimu
Lakini kufanikiwa ni maujanja tu sio lazima elimu
Ili kuyadaka wengine hugeuka wabaya
Mafanikio kwenye kuyasaka wengine hugeuka malaya
Hugeuka was(i)o haya
Kutwa utawakuta kwa babu
Na anayefanya mambo ya maana
Huwa hana muda wa kuyahesabu
Kwenye kuyasaka hakikisha haufilisiki
Haupotezi maisha au vile vitu havinunuliki
Sio kama hatucheki kwasababu tumezeeka?
Nope,ni tunazeeka kwasababu hatujawahi cheka
Tunachukiana? Ndio.
Ila sio sababu kuacha riadha ya mafanikio
Ongeza mbio
Sababu kila mtu, kila kona anasaka mafanikio
Haukungoji wakati. Ooh wewe
Zinapita nyakati.ooh wewe
Muda wako bahati. Oh wewe
Utumie basi... Eeeh eeeh
Una mpenzi (na) uko lonely?
Im sorry ndugu. Haujafanikiwa
Maisha ni kama boli, magoli ndio kufanikiwa
Oooh ooh oooh.oooh. Ndio kufanikiwa
Kila mtu anataka mafanikio...
Hhhmmm. Hhhhmmm. Oh mafanikio
Oh mafanikio
Kila mtu anataka mafanikio



Writer(s): Fareed Kubanda


Fid Q feat. Barakah The Prince - Mafanikio (feat. Barakah the Prince) - Single
Album Mafanikio (feat. Barakah the Prince) - Single
date de sortie
20-01-2019



Attention! N'hésitez pas à laisser des commentaires.