Nedy Music - Acha Iwe текст песни

Текст песни Acha Iwe - Nedy Music



Umenifuta alama ya upendo
Kwenye penzi langu
Tena ukashindwa kuficha matendo
Kwenye mboni langu
Najihisi moyo una ganzi
Ngumu kufika safari yangu
Kinywa kibogoyo silambi
Wala kutafuna
Aliniteka akili yangu
Nikazama mazima mazima
Mwisho wa siku ikala kwangu
Kichwa ikabaki na jina
Oooh yanauma
Ndio maana kila siku shida shida
Tajiri wa huzuni
Ndonda limekosa tiba
Nitapona lini?
Mie eh acha iwe, we acha iwe
Acha iwe, bora nibaki mwenyewe
Acha iwe, we acha iwe
Acha iwe, bora nibaki mwenyewe
Nilishapona kidonda
Ona kaja kukitonesha
Kinywa nong'ona kupenda
Nakosa jibu kuwtwa nakesha
Naumwa kuwaza eh
Huenda pengine moyo hujaridhia
Nyota angaza eh
Mizani nipime wapi nafsi itatulia
Ama ni nuksi mikosi
Nyota ya punda yangu kubeba mizigo
Ninakazana kufosi
Cha jana kuvunda kwangu mi nishazoe
Kila siku shida shida
Tajiri wa huzuni
Ndonda limekosa tiba
Nitapona lini?
Mie eh acha iwe, we acha iwe
Acha iwe, bora nibaki mwenyewe
Acha iwe, we acha iwe
Acha iwe, bora nibaki mwenyewe
Kila siku shida shida
Tajiri wa huzuni
Ndonda limekosa tiba
Nitapona lini mie



Авторы: Chap Kontawa, Said Seif, Said Seif Ally


Nedy Music - Acha Iwe
Альбом Acha Iwe
дата релиза
09-05-2020



Внимание! Не стесняйтесь оставлять отзывы.