Nelly-Music - Mhamiaji Songtexte

Songtexte Mhamiaji - Nelly-Music




Jina langu kanjia potea
Nilikuja ugenini kutembea
Sikujua tunatofautiana
We kiganja na uso vinafanana
Kwenu kumbe matajiiri
Hapa kila jambo linawezekana
Kwetu kila jambo uwezo hatuna
Labda Fedha ama babu hatopenda
Nimeingia nisikopajua
Sina pa kwenda wala sina cha kufanya
Mji Mkubwa kila njia yavutia
Ila kila njia hairudi nyuma
Nashauku ya kutumia uhuru
Uwazi kiasi mimi ndio muamuzi
Kule nyumbani muamuzi ni Mwenyezi
Baba,mama,familia au walezi
Nimepotea
Natafuta njia
Njia ni nyingi nashindwa kuchagua
Nakutafta ewe engineer
Ulie chora ramani ya Dunia
Nina msongo nimesha changinyikiwa
Naona giza nimeshapotea njia
Sijui lugha uoga umeshaingia
Narudi kwetu safari naachilia
Nimejifungia sana
Tamaduni zangu za wakwaza
Ugenini kazi sina
Najiona sina maana
Ninaakuomba unifundishe namna
Ya kuenenda kuishi bila lawama
Nimeshachoka
Kila siku kulałama
Nisaidie njia yenye usalama
Unifundishe kuuliza bila haya
Bila chuki niulize kujifunza
Ninaposhindwa cha kwanza iwe kuomba
Nakusamehe iwe ni jambo la kwanza
Nimepotea
Natafuta njia
Njia ni nyingi nashindwa kuchagua
Nakutafta ewe engineer
Ulie chora ramani ya Dunia
Nimepotea
Natafuta njia
Njia ni nyingi nashindwa kuchagua
Nakutafta ewe engineer
Ulie chora ramani ya Dunia



Autor(en): Nelson Mugarula


Nelly-Music - Mhamiaji
Album Mhamiaji
Veröffentlichungsdatum
10-04-2025




Attention! Feel free to leave feedback.
//}