Bahati - Visa paroles de chanson

paroles de chanson Visa - Bahati



Ni saa moja
Na giza yabisha
Hata bila kujulishwa
Kila mtu nyumbani
Ni saa moja
Na giza yabisha
Mchunguze mwenzio
Macho kwa telly
Ooh
Visa vyaanza
Kila mtu yu kimya
Twangoja vidokezi ooh
Huzuni wajaa hewani
Visa vyaanza,
Kila mtu yu kimya
Twangoja vidokezi ooh
Huzuni wajaa hewani
Na hakuna furaha
Watu wajishika tama
Twalia kwa ndani
Huzuni moyoni
Hakuna furaha
Watu wajishika tama
Twalia kwa ndani
Machozi moyoni
Juu na visa ooh,
Vyatuvunja nyoyo,
'Kifungua macho hautamani uonacho, ooh,
Baba twajiweka
Mikononi mwako
Juu machozi yetu yamekuwa chakula chetu,
Mara baba, kamshika mwanawe kwa nguvu
Mwingine kajitia kitanzi, badala ya mapenzi
Na yule, kasahau nduguye akifuata mali
Sasa ni upanga (kupigania shamba)
Na hili halikosi, vita, kati ya dini
Hatuelewani,
Wakristo, waislamu
Kutwa kucha, tuko vitani
Hatuelewi, hautelewi
Mara ukabila, mara vita, ya mataifa
Hatuelewi, hatuelewi
Ju maskini walia hela, aliyenazo yualilia amani
Hatuelewi, na hatuelewi
Visa ooh,
Zatuvunja nyoyo,
'Kifungua macho hautamani uonacho
Baba twajiweka
Mikononi mwako
Juu machozi yetu, yamekuwa chakula chetu
Visa ooh,
Zatuvunja nyoyo,
'Kifungua macho hautamani uonacho
Baba twajiweka
Mikononi mwako
Juu machozi yetu, yamekuwa chakula chetu
Nchi yetu imekosa amani
Wenzi wetu na bado wakimbizi
Eh okoa Kenya
Mara ukabila eeh
Hatuna usalama Kenya
Tunalia sana
Mungu wetu eeh



Writer(s): Andreas Baertels, Hans-joachim Horn-bernges


Bahati - Lover
Album Lover
date de sortie
19-01-2016




Attention! N'hésitez pas à laisser des commentaires.