Mrisho Mpoto - KItendawili paroles de chanson

paroles de chanson KItendawili - Mrisho Mpoto



Maji ya moto
Kitendawili tega nikutege
Kitendawili tega, tega
Tega nikutege mwiba
Kuku anayetaga hachinjwi, akichinjwa msiba
Sizonjeee
Sizonjee aheee sizonjee
Sizonjeee
Kitendawili
Sizonje aaheee sizonjee
Kumbukumbu yako ikoje katika kukumbuka
Nilikuita sizonje ili uingie ndani
Kwasababu kila anaeingia lazima atoke nje
Sizonje, Sizo Za Nje
Sizonje ahee Sizonjee
Hapa ndipo walipovishana majoho yasiyoonekana
Walisoma hapa, walimaliza hapa
Kila kitu kiliishia hapa
Walipokuja kwetu walituambia
Wale waliosoma na kumaliza
Walimaliza kila kitu wakafa
Kama haujui bahari ilipo tumia mto kwenda
Kitendawili tega, tega
Tega nikutege mwiba
Kuku anayetaga hachinjwi, akichinjwa msiba
Sizonjeee
Sizonjee aheee sizonjee
Sizonjeee
Kitendawili
Sizonje ahee Sizonjeee
Sizonje
Kiukweli watu wanalia
Wapo wanaolia kwa machozi
Na wapo wanaolia kimya kimya
Wapo wanaolia na wanaoendelea kulia
Japo vulio vinatofautiana
Wapo wanaolia kwa kuhisi wamedanganywa
Wapo wanaolia kupoteza ndugu zao
Lakina wapo wanaolia kuona kuna
Msiba kwao Lakini marehemu ndio muandaaji
Wali mweupe kwa shekheee, msiweke nyama za mifupaaaa
Watoto kaeni wanne wanneeee, waandaaji tutakula uwani tena mwishoo.!
Shida zilipohamia shuleni, nikaona nikuwahi kidogo Sizonje.
Mtoto anapoulizwa "Nani atalipa ada?", "baba!" "Yuko wapi??", "kafa!"
Mwalimu wa fasihi anapotoa mfano wa maiti maiti zinazotembea,
Wale watoto wanalia tena
Kwahiyo Sizoo,
Huku nje watu wote wanalia tofauti Lakini msiba ni mmoja
Unaonaje, tuzike kwanza au tuhesabu idadi ya maiti zinazotembea?
Kitendawili tega
Tega nikutege mwiba
Kuku anayetaga hachinji, akichinjwa msiba
Sizonjeee
Sizonjee aheee sizonjee
Sizonjeee
Kitendawili
Sizonje aheee Sizonjeee
Sizonje
Naomba ikumbukwe kwamba, aliyemfundisha Chui kula watu ni binadamu.
Na anayekunyoshea kidole
Kuwanaye makini naye sio muda mrefu atakunasa kofi.
(Sizonje)
Kuku ana hatua tatu katika ukuaji wake
Huachwa kwanza atage, ujue utagaji na wingi wa mayai yake
Tunamsubili atotoe tuhesabu vifaranga na mayai viza
Ndugu zangu, inawezekana kweli tumechoka maharage
Lakini kama tunataka nyama tusubirini kwanja banda lijae.
Kitendawili tega, tega
Tega nikutege mwiba
Kuku anayetaga hachinjwi, akichinjwa msiba
Sizonjeee
Sizonjee aheee sizonjee
Sizonjeee
Kitendawili
Sizonje aheee sizonjee
Sizonje



Writer(s): Mrisho Mpoto


Mrisho Mpoto - KItendawili
Album KItendawili
date de sortie
15-08-2017




Attention! N'hésitez pas à laisser des commentaires.