Mrisho Mpoto feat. Banana Zoro - Sizonje текст песни

Текст песни Sizonje - Mrisho Mpoto



Sizonje hii ndio nyumba yetu
Milango ipo wanapita madirishani
Sizonje ndio nyumba yetu
Milango ipo wanapita madirishani
Ingia uyaone, maajabu ya nyumba yetu
Ingia uyaone, maajabu ya nyumba yetu
Tulikaa barazani, tukasikia kelele
Kelele toka ndani,
Mtu anaruka dirishani
Sizonje, karibu nyumbani kwetu
Uone maajabu ya nyumba yetu
Karibu sana Sizonje,
Hii ndio nyumba yetu,
Tulipoficha mundu za kupondea wezi,
Kwani, makaburi yaliofukuliwa lazima yazikwe upya.
Nyumba hii Sizonje ina vyumba vinne,
Vitatu havifunguki,
Kimoja hakina mlango,
Japo kuwa kina watu ndani, na hawaongei kiswahili,
Wenyeji wanalala sebleni na walishazoea,
Sizonje kule tulipotoka panaitwa jikoni,
Huna haja ya kwenda kule,
Kumejaa mafundi wa kupika
Sasa hivi wanakupikia wewe ili ule ulale
Ukiamka muongee nini hasa ujio na dhima ya safari yako
Wanashangaa mbona ghafla
Samahani sana mgeni
Wapishi wameniomba kwamba Nikuulize tena kwa
Kukuomba kwamba Eti unapenda vya mafuta au vya nazi?
Wanataka kukuonyesha madoido katika mapishi yao Sizonje
Sizonje chumba hiki naomba usiingie Ukimaliza nitakwambia kwanini
Kuna sauti inajirudia mara kwa mara
Na hapa mlangoni kulikuwa na picha mbili kubwa
Moja picha, nyingine mchoro wa picha wa kwanza
Ninachokumbuka iliwahi kuandikwa "USIYEMTAKA KAJA"
Hatukuwahi kuelewa maana yake
Labda kwa sababu ya ujio wako unaweza kutusaidia
Sizonje hii ndio nyumba yetu
Milango ipo wanapita madirishani
Sizonje hii ndio nyumba yetu
Milango ipo wanapita madirishani
Ingia uyaone, maajabu ya nyumba yetu
Ingia uyaone, maajabu ya nyumba yetu
Najua, wimbo mbaya haufai kubembelezea mtoto
Na kamwe mtoto hawezi kuungua Kwa kiazi
Kilichokuwa kwenye kiganja cha mama yake mzazi
Njoo huku uone Sizonje Si unajua,
Harufu ya uzazi haiishi mpaka mtoto akue Sawa,
Sizonje, huu hapa ni ua
Lile pale ni shimo la taka
Na kile pale ni choo
Kinachotutisha na kutuogopesha zaidi Wanaoishi humu ndani
Hawajawahi kutupa taka Wala kwenda chooni
Kama ukiwa makini Kwa nje utasikia sauti za makundi ya watu
Wengi ni vijana,
Wana bahasha za khaki mikononi
"KAMA HAMTUPI TAKA SHIMO HILI MLICHIMBA LA NINI?"
Lakini pia kwenye sauti zao, Sizonje Kuna watoto, Wazee na kina mama
Ukiunganisha sauti zao ndio unapata hizo kelele
Ninavyosikia, Ila sina uhakika
Waliambiwa kihistoria nyumba hii ni ya kwao
Na wana haki ya kutupa taka na kutumia choo hiki
Sasa, njoo nikuonyeshe huku uchochoroni Uone maajabu Mengine ya
Nyumba hii Sizonje, ukiona tembo anaringa Ujue mvua zinakaribia
Sizonje hii ndio nyumba yetu
Milango ipo wanapita madirishani
Sizonje ndio nyumba yetu
Milango ipo wanapita madirishani
Ingia uyaone, maajabu ya nyumba yetu
Ingia uyaone, maajabu ya nyumba yetu
Ingia uyaone, maajabu ya nyumba yetu
Ingia uyaone, maajabu ya nyumba yetu



Авторы: Mrisho Mpoto


Mrisho Mpoto feat. Banana Zoro - Waite
Альбом Waite
дата релиза
30-11-2015




Внимание! Не стесняйтесь оставлять отзывы.