Proffesor Jay - Jina Langu текст песни

Текст песни Jina Langu - Proffesor Jay



Jina langu linavuma kwenye mitaa
Jina langu lina hadhi ya kisupa staa
Jina langu linaongeza idadi ya maadui
Wengine nawajua wengine siwatambui
Jina langu.kwikwi eyo J tunakuzimia
Jina langu.J alosto ameshazeeka
Joseph Haule mc shupavu wa mitulinga
Mchawi wa rhymes mti mkavu
Macho ya chinichini yanatizama nyendo zangu
Najua hiyo yote sababu ya kipaji changu
Sitaki kujua nani adui nani mwenzangu
Na kwako muumba wangu ongeza hekima kwangu
Hiyo sipo ukingoni miguu nje maji ya shingoni
Mwenye tungo badili wamejizika shimoni
Nani kabaki wapo kitaani mshumaa hauwaki
Wameshindwa kuikabili fataki za itifaki
Vina vyangu mahili kwenye giza kama kandili
Na kwenye vichwa vya wapotevu naacha kitendawili
Ni J mti mkavu niite nyota nyang'avu
Inayopigwa vita na wenye hoja chakavu
Bado nachakarika na naona kaa za njoshi
Eeh!! mola ni lini itakwisha hii mikosi
Najuta kuitwa supa staa naona karaha
Mangurubange na washikaji yananigasi nashangaa
Huu ni mtafaruku na kero kwenye mitaa
J njoo baba ni better tuvute raha
Weka mapenzi kando nipeni hoja za msingi
Wangapi mtanipenda nikiwa sina shilingi
Jina langu linavuma kwenye mitaa
Jina langu lina hadhi ya kisupa staa
Jina langu linaongeza idadi ya maadui
Wengine nawajua wengine siwatambui
Jina langu.kwikwi eyo J tunakuzimia
Jina langu.J alosto ameshazeeka
Joseph Haule mc shupavu wa mitulinga
Mchawi wa rhymes mti mkavu
Thamani ya ubongo wangu ni kubwa kuliko bingo
Nashangaa mapromota bado mnaleta maringo
Bado napiga goti kwa mungu aniongezee
Kwenu vijana wa bongo poleni na starehe
Jasho langu la chuma lataka moyo kulila
Na wote mtabana ngenge wachawi na wenye hila
Nimeshasebenza na shuluba nyingi za maisha
Kumbukumbu tu ninazo mr ticha .mr ticha
Wape hi marekani wabongo mashabiki wa mbali
Bongo dar es salaam mitego bado si shwari
Ninapokosa hela washikaji wanatoweka
Ninaporekebisha pumbavu wanasogea
Naamini akili yangu ina akili kuliko mchwa
Na ninajua hoja mpya ndo siku inapokucha
Mwanga na saluti kumkoma nyani jirani
Bado nipo makini siogopi mpinzani wa jadi
Maneno yangu yajivu ni kama muarobaini
Jamii inakubali vibwengo chomeni chini
Wapo baadhi ya watu wanaotaka kunihukumu
Wanatamani ningekuwa sioni waninyweshe sumu
Wengi wananipenda wachache hamnipendi
Skendo mnazonipa na mimi sipendi
Mbio zipo ukingoni chomeka mbavu za mbwa
Na chochote mnachosema bab kubwa
Jina langu linavuma kwenye mitaa
Jina langu lina hadhi ya kisupa staa
Jina langu linaongeza idadi ya maadui
Wengine nawajua wengine siwatambui
Jina langu.kwikwi eyo J tunakuzimia
Jina langu.J alosto ameshazeeka
Joseph Haule mc shupavu wa mitulinga
Mchawi wa rhymes mti mkavu
J tunakuzimia at yahoo dot com
Pande zote nitakwenda lakini bongo ndo hom
Nazidi kuumiza kichwa nazidi kupata wafuasi
Maisha ya starehe na ngono kwa sasa basi
Nafungua milango kwa ajili ya kizazi kipya
Na chance bado ipo wazi kwa wote waliojificha
Kwenye matamasha nilidhulumiwa mshiko
Mapromota walikimbia kabla ya kufanya malipo
Sasa jino kwa jino nakwenda nao sambamba
Napotembea haki siogopi nani katanda
Leo nathibitisha ya kwamba kweli natisha
Ni fukuto ulanjonjo kwa wote wanaobisha
Fukara wa kipato nina akili za kitajiri
Na muda utakapozidi naamini wote mtakiri
HBC muongozo wa ma-mc kamati kuu ya wanga imebi
Jina langu linavuma kwenye mitaa
Jina langu lina hadhi ya kisupa staa
Jina langu linaongeza idadi ya maadui
Wengine nawajua wengine siwatambui
Jina langu.kwikwi eyo J tunakuzimia
Jina langu.J alosto ameshazeeka
Joseph Haule mc shupavu wa mitulinga
Mchawi wa rhymes mti mkavu



Авторы: Joseph Haule


Proffesor Jay - Machozi Jasho Na Damu
Альбом Machozi Jasho Na Damu
дата релиза
03-03-2001



Внимание! Не стесняйтесь оставлять отзывы.