Zuchu - Nimechoka текст песни

Текст песни Nimechoka - Zuchu




Lalalalala Lalala Lalala
Ooh ooh ooh
Umenijengea kumbukumbu mbaya kwenye penzi lako
Siwezirudi hata nishikie bakoraa
Nanena kwa machungu umentendea vibaya mi, mwana mwenzako
Kwa makusudi furaha umenipora
Aah, asante umenifunzaa
Nionapo njia mbili nichague yakuvuli
Mimi,mi sio wa kwanza kuumizwaa
Wanatendwa matajiri, sembuse mi wa sifuri
Aah,na nakujua kwa kumsingizia she kwani
Huyo ni wewe, ni wewe, ni weewe
Ukinikumbuka usijipigishe u-turni
Uniache mwenyewe, mwenyewe, mwenyewe niache
Nimechoka, nimechoka
Nimechoka, baasi
Nimechoka, nimechoka
Nimechoka, baasi
Eh,hasira
Hasira ndo maradhi yangu
Hasira
Nimepoteza muda wangu jamani hasiiira
Hasira ndo ugonjwa wangu
Hasira
Nimepoteza lengo langu
Sitamani sitamani makosa niyarudie
Isiwe desturi yangu kuuchuza moyo uumie
Bora nirudi nyumbani Pemba wanitambikie
Nifungwe akili yangu, mawazoni nikutoe
Ooh maana nakujua kwa kumsingizia she kwani
Huyo ni wewe, ni wewe,ni weewe
Ukinikumbuka usijipigishe u-turni
Uniache mwenyewe, mwenyewe, mwenyewe niache
Nimechoka (nimechoka), nimechoka (nimechoka)
Nimechoka, baasi (we shika zako nami nishike zangu)
Nimechoka (nimechoka), nimechoka (nimechoka)
Nimechoka, baasi





Внимание! Не стесняйтесь оставлять отзывы.