Fid Q - Mwanamalundi Lyrics

Lyrics Mwanamalundi - Fid Q



Mwanamalundi!
Ah
Niite ngosha the don, niite mwanza mwanza
Love me. or leave me alone
Nakipakaza unaposema hukomi, nami
Simwoni wa kujitandaza juu, ya kitanda hiki cha mziki
We hujui utanishangaza, wanakoshwa!
Masikioni wanaposikia hizi ladha
Inawachosha inavyo'hit redioni nyomi inajaza
Mashabiki, zaidi ya milioni hadi wakusaza dah
TMK, Ilala na 'Ndoni wanamjua mwanza
Ambaye ame'base na hiphop kama saigon wa zavaragwanza
Naenda mlipa kama scratch zina bony love jibaba homie
Na'keep on top, Mcee slash hustler
Kwenye hip naweka hop kisha naiteka ki'mafia
Chapchap. nonstop hits je we utabaki.
Jinsi nnavyozi'drop machizi, chicks wanafagia
Tamu kama lollipop, rhymes nnazoshusha
Situmii kalamu, kichwani hapohapo natungia
Natumia ufahamu wa hii fani, maisha kuyashuhudia
Naangalia angani naona amani inaniambia dereva ntabeba msalaba begani usukani nikiuachia
Niite Ngosha the don, au
Mwanza Mwanza au
Mwanamalundi
Mwanamalundi
Mwanamalundi
Mwanamalundi
Kuna makeups, pia mkorogo
Kuna haters, na wale waliojiskia tu kuleta shobo
Kuna tofauti kati ya Mcee na CEO,
Tambi na minyoo
Glass na kioo
Bafu na choo
SKIA, ili usisahau
ONA, ili ujifunze
FANYA ili ukumbuke kama ulisahau ya jana
Wafurahishe walio karibu, walio mbali watasogea
Elewa, kama mbwa, usijaribu hata kuongea
Unachokitaka haukipati, aliyekipata hakitumii
Hapo ndipo utapodata na mashauzi ya plan b
Mikakati ya kiusanii na wakati wa bahati nasibu
Sio lazima kipaji ili mradi mshakaji anahitaji kitu
Atasukumaje siku?
Huyu mzugaji mzinguaji siwezi kumpa
Huyu wakati Mungu ndo mpaji, unakosea hii
Wanatumia mbaya za bandia kurudia viporo
Ushapagawa, watoto sasa wanasaka chochoro
Hapa kahawa, ni maji ya moto yenye rangi ya ugoro
Hatuwezi kuwa sawa, mwendo wa kasoro zenye kasoro
Uhuru wa miguu mikono, akili imefungwa mnyororo
Ntawadhuru sana huo usingizi wa pono tommorrow
Hauna ushuru mdomo, chunga ulimi usilete mgogoro
Ona, bila farasi kidume hawezi kuitwa Polo
Niite Ngosha the don, au
Mwanza Mwanza au
Mwanamalundi
Mwanamalundi
Mwanamalundi
Mwanamalundi



Writer(s): Fareed Kubanda


Fid Q - Propaganda
Album Propaganda
date of release
19-03-2011




Attention! Feel free to leave feedback.