Young Killer - Mungu Baba Lyrics

Lyrics Mungu Baba - Young Killer



Asante babaa
Kwa pumzi ya buree
Ninayoitumia kwenye dunia
Haaaaahh
Asante Molaaaa
Huuuuuu
Umenipa pumzi bure
Nikawika jogoo
Kabla sijamjua huyu na yule
Ukam-bless mama kisha akanizaa kwa uchungu
Nlibahatika kuwa salama kwa uwezo wako Mungu
Umenipa uwezo mkubwa wa dunia
Mboni macho na masikio
Ili niweze kuona na kusikia
Pia akili ya kufikiria
Ukaniongeza pia na mdomo
Ili niwashukuru wanaonisifia
Ukaleta dini
Ukaleta mapadri na mashee
Na maandiko ile tuamini ni wewe pekee
Mwenye mamlaka na vitu vyote vilvyomo ndani
Tukiwa na huzuni basi tuongozwe na burudani
Tupendanee
Ukatupa maua yanayonukia
Uwezo wa kukimbia hatari ingia
Ukatupa na hisia na uchungu tukisikia tunalia
Ukaweka mchana mwanga
Usiku tulale giza likiingia
Ukaweka kifo kukumbusha hatuishi siku zote
Popote nilipo basi nikuabudu muda wote
Sisahu kuwa Mungu ni wewe
Sisahau marafiki ndo watanizika na wataniacha mwenyewe
Naishi napumua ni upendo wako
Mungu baba
Chini ya jua ni kwa uwezo wako
Mungu baba
Naishi napumua ni utashi wako
Mungu baba
Heeee
Mungu babaaa
Eeeehhh
Mungu baaaa
Yeeeeehhh
Ukaumba matajiri haswaa ukawapa note
Ukampa jina mamaa aniite Erick Msodoki
Ukaweka jua lenye joto tulione mbaliii
Ukaweka mvua ukaweka moto ili tupike ugali
Umetupa ujasiri tuamini we special
Umewapa watu akili lakini wasijue kesho
Fisi anakula mifupa
Paka umempa roho saba
Nimezunguka nimeamini hakuna kama wewe baba
Umeumba wakristu
Baba
Umeumba waislam
Baba
Umeumba hadi wale wanaoabudu masanamu
Baba
Umeweka pepo
Baba
Umeweka jehanam
Baba
Umeumba wajinga
Baba
Umeumba timamu
Baba
Umemuweka hadi shetani anayefanya tukusahau
Umeweka anasa duniani zinazofanya tujisahau
Umetupa imani tujue Mungu ni mmoja
Na malipo ni duniani na tunaishi mara moja
Naishi napumua ni upendo wako
Mungu baba
Chini ya jua ni kwa uwezo wako
Mungu baba
Naishi napumua ni utashi wako
Mungu baba
Heeee
Mungu babaaa
Eeeehhh
Mungu baaaa
Yeeeeehhh
Ahhhhhh
Ni kweli Mungu aliumba ulimwengu
Kisha akatuumba wanadamu
Na kama haitoshi akatupa pumzi ya bure
Ili tumpende
Tumtumikie
Tumuabudu
Na siku moja tufike kwake binguni
Eeeh Mungu tufanyie wepesi
Na utuzidishie pale tulipopungukiwa
Kila mwenye pumzi na aseme
----ameeeeeeen-------



Writer(s): Young Killer


Young Killer - Mrs. Superstar
Album Mrs. Superstar
date of release
05-11-2015




Attention! Feel free to leave feedback.