Young Killer feat. Banana Zorro - Umebadilika Lyrics

Lyrics Umebadilika - Young Killer feat. Banana Zorro



Pokea busu shavuni
Toka kwa mnyamwezi
Ambaye uliona nakurubuni
Mdanganyifu wa mapenzi
Leo umeniona kanuni
Bila mimi jibu huwezi
Chozi mwanzo wa huzuni
Maji ndo huleta utelezi
Sasa unalala salama
Unakumbata picha yangu
Usiku njozi zinakwama
Bila sauti yangu
Leo zamu yako, mama
Si unakumbuka hustle zangu
Kipindi unanitukana
Ukidai sio type yangu
Sasa unaniita mchumba
Unaamini nitakuoa
Hadi macho unanifumba
Hata tongotongo sijatoa
Unanipa hadi mavumba
Nisifulie nikaboa
Unamshukuru Muumba
Zawadi ka mimi kuitoa
Si ulinisema kwa babako
Anikamate, aniadhibu
Ukiwa na wenzako
Mkiniponda kwa zabibu
Haukujua nitakuwa wako
Nitashinda majaribu
Ingawa mwaka mzima nilihustle
Nikufate ili unipe jibu
Ni nini kilichobadilika?
Ni nini kilichokubadilisha?
Ama ni mimi nimebadilika?
Siamini mi, umekamatika
Umeshikika, umebadilika we
Ah, yaani ule utumbo ulioutupa
Ukanipa nikaulia ndizi
Mpaka pande za fukwe
Tukasepa kubarizi
Hauna shauku pale unapoona machizi
Eti unampenda Belle na Ice ndo wapo easy
Unanipa ushauri
Pamoja tunaujadili
Ukasema una nafsi moja
Hauwezi kutupenda wawili
Nafasi niliyonayo kwako
Zaidi ya kunipa mwili
Sa ni ndoa hitaji lako
Eti umechoka kusubiri
Sasa haulali hadi unipigie phone
Unadai nina kosa kubwa la kutesa moyo wako
Naheshimu hisia zako
Unavyosema unaniamini
Hata vocha ya laki moja
Haitoshi kuongea na mimi
Mapenzi yangekuwa ni maji
Nahisi ungenipa bahari
Mapenzi yangekuwa kipaji
Nahisi ungenipa mistari
Hauhitaji ushauriwe juu yangu
Mwamuzi wewe
Unasema moyo wako, wangu
Na mi ndo chaguo la wewe
Ni nini kilichobadilika?
Ni nini kilichokubadilisha?
Ama ni mimi nimebadilika?
Siamini mi, umekamatika
Umeshikika, umebadilika we
Ah, nimekupa nini, unadai
Tofauti na sauti nzuri niliyokuimbia kitandani
Daily unafurahi
Ama ni swagger za majeans na tai
Ama ni penzi zuri n'nalokupa asubuhi kabla ya chai
Umechoka kuniita Killer
Unataka uniite mume
Mapenzi yangekuwa ajira
Ungeniajiri kidume
Nishakuteka fikira
So inabidi tu ujitume
Kuniweka sawa kisha
Tuwadhibiti paka shume
Unasema ungejua mapema
Hata usingeringa
Ungenipokea kwa moyo mmoja
Mikono ungekinga
Kwa kiss za kutosha
Ungenihug kila saa
Na kama ungekuwa malkia
Ungenihonga hata Dar
Sikufichi, mama
Unanipa raha
Nimeshinda vita yako ya mapenzi
Na sitojiita shujaa
Sihitaji nishauriwe juu yako
Mwamuzi mimi
Nasema moyo wangu, wako
Na we ndo chaguo la mimi
Ni nini kilichobadilika?
Ni nini kilichokubadilisha?
Ama ni mimi nimebadilika?
Siamini mi, umekamatika
Umeshikika, umebadilika we
Ama nyimbo za mapenzi zimekubadilisha?
Maneno yangu ya mahaba
Mpaka umebadilika
Siamini mi, umebadilika
Umeshikika, umekamatika we
Man Walter and D Classic
Msodoki



Writer(s): Young Killer


Young Killer feat. Banana Zorro - Mrs. Superstar
Album Mrs. Superstar
date of release
05-11-2015



Attention! Feel free to leave feedback.