Rayvanny - Vumilia paroles de chanson

paroles de chanson Vumilia - Rayvanny



It′s Bob Manecky
Iyee, iyee iye eh
Iwe kibatari, ama mwanga wa mshumaa
Kwenye kigiza cha jioni
Pika dona ngangari, tulishushie na dagaa
Ukishatoka sokoni
Kisha tufunge safari, itayochukua masaa
Utokwe jasho mgongoni
Na vile 'na machachari
Nikikushika Kibaha, utamu hadi Kinondoni
Kuna muda nawaza, hivi nitakupa nini?
Sina mbele sina nyuma masikini
Chakula shida na tunalala chini, nambie
Wenye mapesa, Vogue na ma-Lamborghini
Wasijefanya ukanipiga chini
Bado nawaza, hivi nitakupa nini utulie?
Sambusa, kachori, bamia (aah)
Tukipata pesa ni sangara
Mchicha, mtori, bamia (aah)
Kama tukikosa tunalala
Kwa hiyo mama usijali, vumilia (iye eh)
Vumilia (iyee ye)
Vumilia, kesho tutapata mpenzi
Vumilia (vumilia)
Vumilia (vumilia)
Vumilia, kesho tutapata mpenzi
Najua unatamani high waist, make up
Weaving za Dubai na China
Ule pamba nyepesi, setup
Cheni ya dhahabu yenye jina
Basi mama vumilia, nakupigania, mpenzi subiria
Acha kujiinamia, punguza kulia, atatusaidia
Eti mapenzi si moyo, mapenzi ni pesa
Ama kweli masikini yatatutesa
Uchoyo, usinipe presha
Naomba unipende
Kuna muda nawaza, hivi nitakupa nini?
Sina mbele sina nyuma masikini
Chakula shida na tunalala chini, nambie
Wenye mapesa, Vogue na ma-Lamborghini
Wasije fanya ukanipiga chini
Bado nawaza, hivi nitakupa nini utulie?
Sambusa, kachori, bamia
Tukipata pesa ni sangara
Mchicha, mtori, bamia
Kama tukikosa tunalala
Kwa hiyo mama usijali, vumilia (iye eh)
Vumilia (iyee ye)
Vumilia, kesho tutapata mpenzi
Vumilia (vumilia)
Vumilia (vumilia)
Vumilia, kesho tutapata mpenzi



Writer(s): Raymond Mwakyusa


Rayvanny - Flowers
Album Flowers
date de sortie
08-02-2020




Attention! N'hésitez pas à laisser des commentaires.