Darassa feat. Rich Mavoko - Segedance (feat. Rich Mavoko) текст песни

Текст песни Segedance (feat. Rich Mavoko) - Rich Mavoko , Darassa



Ana ngoma zote samba vanga sidimba
Ukiingia anga zake rare timba
Hadithi hadithi utam kolea
Huwezi kusimulia mvua haijakunyeshea
Take care huu sio moto wa kuotea
Mimea juba mbovu litakubomokea
Usimchokoze mwache komando kalala
Akiamka biashara shaghala baghala
Mtu hasara wamezinga mabomu Mbaghala
Akitinga home anaacha msala
Kaamkia stand hata bila safari
Kashazima zake data hana habari
Kutwa za watu machata kujikubali
Mastaa plasta mtu wa ajali
Nitakuingiza chaka usimweke dhamana
Alikolala leo sio huko aliamka jana
Hana usiku hana mchana hana maana
Mtu lawama hana team hana chama
Unakuja kutaste taste weka anachomeka
Kama unabet bet anachana mkeka
Wameshikwa na baridi wanatetemeka
Wamepatwa na mawenge wanaweweseka
Huyu bwana hana mzaha anapiga honi
Tena kabeba silaha kali kibindoni
Sema suto na vumbi usoni
Tia mguu uende na maji mtoni
Anazijua njama, drama, utampenda
Anakuwa mnyama ukiinama
Ukiinuka amekwenda nawe eeh
Mzee wa segedance
Kukaba kuiba kashazoea, segedance
Wanamuita segedance
Dhuluma kupiga nyumbani, segedance
Siku nyingine kumekucha kwenye misele
Ye anawaza mbele maisha yatakuwa mtele
Stori zake chenga chenga nyingi kama Pelle
Kwa vitambo hajambo majigambo tele
Tunaishi naye kimatale mtaani
Ukasero kwake yeye ni kama maskani
Umri wake na matendo haviendani
Jua kali cheki mwendo shati begani
Akiingia party kaharibu kaishia
Sio mtu kweli bandia bandia
Mambo yake ni kudandia dandia
Mkate anashushia na bia
Kichwa imewaka ti na anapepesuka
Hana muda wa kuoga anapaka mafuta
Mueke vigingi chimba chimba na matuta
Hutomkuta maajabu ya Musa
Unakuja kutaste taste weka anachomeka
Kama unabet bet anachana mkeka
Wameshikwa na baridi wanatetemeka
Wamepatwa na mawenge wanaweweseka
Huyu bwana hana mzaha anapiga honi
Tena kabeba silaha kali kibindoni
Sema suto na vumbi usoni
Tia mguu uende na maji mtoni
Anazijua njama, drama, utampenda
Anakuwa mnyama ukiinama
Ukiinuka amekwenda nawe eeh
Mzee wa segedance
Kukaba kuiba kashazoea, segedance
Wanamuita segedance
Dhuluma kupiga nyumbani, segedance




Darassa feat. Rich Mavoko - Slave Becomes A King
Альбом Slave Becomes A King
дата релиза
24-12-2020



Внимание! Не стесняйтесь оставлять отзывы.