Kidum Kibido feat. Sana - Mulika Mwizi (Remix) текст песни

Текст песни Mulika Mwizi (Remix) - Sana , Kidum Kibido



Yuuuuuh tarararah
Ukiona mwanaume kwa hali ya kulia
Ujue kwamba ameguswa pahali
Sio rahisi si kawaida kushuhudia
Mwanaume akitoa machozi
Hapo zamani nilidhani
Mwanaume akipoteza kazi ndio uchungu ndio unyonge
Kumbe mapenzi ndio sumu kali
Inayofanya mwanaume kulia kama mtoto
Kama kibogoyo
Habembelezwi, hanyamazishwi
Machozi yake inatoka ikienda tumboni
Habembelezwi, hanyamazishwi
Machozi yake inatoka ikienda tumboni
Mulika mwizi (mulika na tochi mulika)
Mulika mwizi (kama kuna giza mulika)
Nimulikie mwizi, nasumbuka nataka kujua
Nani mwizi wa mapenzi?
Kwa barua pepe kwa simu ya nundu
Ujumbe mfupi unafutwa kwa sekunde tatu
(Sekunde tatu), nilimpenda baby wangu
Nikampea Roho yangu
Amechukuliwa, amenyakuliwa
Kama fulani apa mtaani
Mwenye magari na mapesa amechukua baby
Ikanifanya crayz
Sibembelezwi, sinyamazishwi
Machozi yangu inatoka ikienda tumboni
Nisiomboleze? Ninamjua huyu jamaa
Anajifanya bubu wengine vipofu
Mulika mwizi jamani (mulika mwizi)
Nimulikie mwizi (mulika mwizi)
Nimulikie mwizi, nasumbuka nataka kujua
Nani mwizi wa mapenzi?
Nani mwizi wa mapenzi?
Ukiona baby wako anaingia kwa bafu na simu mkononi
Huyo ni mwizi (mulika mwizi)
Ukiona mzee wako anazima simu kila mara akiwa kwa nyumba
Mulika mwizi (mulika mwizi)
Ohoooo oh, ohooo oh, oooooh
Ohoooo (nimulikie mwizi jamani) ohh
Mulika mwizi, nionyeshe niambie ni wapi?
Mulika mwizi, mwizi wa mapenzi, mwizi wa mapenzi
Mulika mwizi, nani mwizi wa mapenzi (mulika mwizi)
Nani mwizi wa mapenzi (nimulikie mwizi)
Yu waniua (mulika mwizi), you waniumiza
Ohhh (mulika na tochi) oh
Tazama mbele, tazama nyumba
Kila mtu mwizi wa mapenzi
Kila mtu mwizi wa mapenzi
Pia mimi mwizi wa mapenzi.



Авторы: Jean-pierre Nimbona


Kidum Kibido feat. Sana - Kidum: Collection, Vol. I
Альбом Kidum: Collection, Vol. I
дата релиза
26-02-2017



Внимание! Не стесняйтесь оставлять отзывы.