Stereo - Hitaji Lyrics

Lyrics Hitaji - Stereo



Kama utani ukala kona
Yangu macho na siamini ninachokiona
Wala ninachosikia itasema hisia
Inaniumiza mbona umeniadhibu bila hatia
Nafikiria natamani kulia
Kila nikisoma ujumbe wa mwisho ulionitumia kwamba muda umewadia
Tamati imefikia swali najiuliza
Kwanini mapema ukuniambia
Mapenzi tulianza tangu tupo form three
Leo umenitosa najua huko happy upo free
Hauko nami tena nani nitamuita the one only
Sina cha kusema zaidi nimebaki lonely
Siwiki mjini mi jogoo la shamba
Umenipiga chini na umenifundisha kwamba
Tunda likianguka chini ndoto kurudi mtini
Zaidi ya mama mzazi msichana yoyote simuamini
Koche kwa chambers uliona kama kituo cha polisi
Umeniacha solemba mbona umevunja promise
Rafiki zako walishtuka walivyosikia
Hauko na nami shori imebaki stori nawahidithia
Wapi victory limebakia pengo tungeandika history tungefikia lengo
Umeniongopea kilichotokea sikutaraji
Wapi umeelekea nafsi bado inakuhitaji
"Chorus...☆"
Nimekoma sababu umenikomesha
Moyo umenichoma ki ukweli umenikondesha
Umeleta msiba sijui matanga yataisha lini
Umeshika mpini nitafanya nini maskini mimi
Sina uhakika imefutika ndoto ile
Lini ntafarijika naunganika na kachile
Kuishi maisha bila kuna vingi namiss
Kwanza moja mimi mwenyewe sio kitu rahisi
Kama adhabu nishaadhibika adabu nishaadabika katika
Dunia ya love sina uhakika wakupenda mwengine we jaribu pengine
Niweke wazi tu umepata bwana mwingine
Mi sio handsome labda unataka mabraza men uniite
Managenii moyoni inanipain zari haukuwa maharage soya
Sina mali ila penzi la dakifoya
Ila unatambua basi tu umenifelisha
Wewe si yule ninaye kujua nani amekubalisha
Inanisikitisha hamna maposition
Ntafanya nini sasa zaidi kurespect your decision
Sikuchukii mema nakutakia ukiona umepotea njia unaweza ukarudi pia
Ntakupokea ntasahau yalitokea sintobalika zaidi yule yule nitabakia
Kumbuka enzi tumeshafanya mengi sana
Ngumu kuamini sasa yote hayana maana
Naamini muda utasema utarudi lini
Nakupenda daima mpaka siku nafukiwa chini
"Chorus..."



Writer(s): stereo


Stereo - African Son
Album African Son
date of release
01-06-2015




Attention! Feel free to leave feedback.