Harmonize - Imani текст песни

Текст песни Imani - Harmonize



Mmmh mmh
Imani nafsi inaniambia
Haukuwa fungu langu
Na sidhani kama nilikosea
Kuukabidhi moyo wangu
Ulinidanganya mapenzi ni zuri basi
Panda twende safari
Bila kujua la kwako ni mwendo kasi
Ghafla ukanipa ajali
Upweke umetawala nafsi
Mwenzako usiku silali
Ninahesabu mabati
Kisa wewe
Sijutii moyo wangu
Kupenda nisipopendwa
Sirudii makosa yangu
Ujinga wakati wakwenda
Kinachoniuma roho yangu ooh
Kuwapa neno wahenga
Maana si kwa posti zangu
Na kujinadi napendwa
Nishapona, nishapona
Nishapona ila mazoea
Basi nenda umwambie
Nishapona!
Oooh mwambie (nishapona)
Basi umwambie eeh
Nishapona ila mazoea
Heshima kumnyenyekea
Nilivyomnyenyekea
Akaniona si chochote kwake
Mazima akanipotezea
Akanipotezea, alipomaliza shida zake
Ila bado siamini kweli ndo yule
Alokuwa akisema, halali asiponiona
Na kujilisha yamini, yote ni bure
Nikamwita chanda chema, alinidanganya
Zile miziki za kunichombeza, zinaniuma roho
Mara akinidekeza, elaji njoo
Ungesema nilipoteleza, nikamwomba poo
Si vyema amenitelekeza eti kisa roho
Basi nenda umwambie, nishapona!
Oooh mwambie, nshapona
Basi umwambie eeh
Nishapona ila mazoea
Basi nenda umwambie, nishapona!
Oooh mwambie, nishapona
Basi umwambie eeh
Nishapona ila mazoea
Nenda kamwambie naja
Nenda kamwambie naja
Basi nenda kamwambie naja
Nenda kamwambie naja




Harmonize - Kwa Ngwaru
Альбом Kwa Ngwaru
дата релиза
27-11-2019




Внимание! Не стесняйтесь оставлять отзывы.