Fid Q - Juhudi Za Wasiojiweza текст песни

Текст песни Juhudi Za Wasiojiweza - Fid Q




Juhudi za wasiojiweza
Huu moyo huficha siri ambazo kwa macho huzioni
Kwa kuwa mi sio mchoyo ntakupa jambo jipya sikioni
Fedha zao ni nyingi nyingi zaidi ya akili zao
Hawaskizi shida zako za msingi na wao wana zao
Mnazi haupandwi kwa ukucha na hupanda ngazi hushuka
Kuteleza sio kuanguka mbaya ukishindwa kunyanyuka
Anayefanya hajui chochote anayejua hawezi fanya
Ambaye amechoka kufikiria huamini anajua sana
Kama haujutii ya jana na pia hauohofii ya kesho
Unaweza kuyapatia kimaisha yeah au kuyaotea
Unataka kuchukiwa na mjinga mwambie akikosea
Ukweli siku zote unapigwa pingu uongo uzidi enea
Wenye nia hawana nguvu na wenye nguvu hawana nia
Wanaridhika na moja wanaogopa kutafuta mia
Wanayafokea maji wakati wanaogelea
Ukiwakosea hawa press charges vidole vyao vimeenea
Uzembe umewafelisha wengi na bado wengi wanatega
Wanaumia hii dunia imewaangukia juu ya mabega
Na wakilega, wanakosa hata food juu ya meza
Sina budi waeleza hizi ndo juhudi za za wasiojiweza
Umewafelisha wengi na bado wengi wanatega
Wanaumia hii dunia imewaangukia juu ya mabega
Na wakilega, wanakosa hata food juu ya meza
Sina budi waeleza hizi ndo juhudi za za wasiojiweza
Moyo nakwambia, tizama ukiusikia
Usicheze na nyunda asiyejua usi
Mzoea punda hapandi farasi
Hapandi farasi kwake si mzuri
Japo mda beach nguo za hariri
Kuona najisi si yake fahari
Si yake fahari kweli nakwambia
Ngulu kwa ugali ameizoea
Ziwa kwa sukari ukimpa hulia
Ukimpa hulia akasikitika
Dodo hujitia kayatapika
(Juhudi za wasiojiweza)
Wanajifanya wanaleta msaada, kumbe wanaingiza madawa
Mtwara tutakula wapi ndo kundi la kwanza kupagawa
Wanatumia antidote kabla ya kukumbana na sumu
Kuanzia nyayo hadi utosi nje ndani utajilaumu
Hata dunia iki change vipi paka hawezi taga mayai
Na ukiyachemsha au kuyakaanga hupati vifaranga why
Wanamrudisha ndani ya maji samaki aliyekufa afufuke
Kamba iliyolegea kama una haraka usiivute
Dini zinageuzwa kuwa biashara kubwa kubwa huwezi amini
Wanajaribu kutuangusha wanakuta tushalala chini
Kuna masikini na ombaomba wanaogeuza kidonda mtaji
Kuna ukimwi na siamini wagonjwa ndomu waliitumiaje
Anayezijua lugha tofauti kote atapaona nyumbani
Fanya uzijue na kona zote kama ufagio wa zamani
Amani ilileta pesa pesa imeleta vita
Hawazingatii mauzo ya wasaniii baada ya kulipwa
Ni vyema kumpenda mkeo siri zako mwambie mama ako
Usije muonyesha utupu mkweo kisa umelewa itakua aibu yako
Mlevi kesho yake hujuta zinapomruka hana hata jiti
Au labda alipigwa chupa bar za siku hizi ugomvi wa viti
Mc mkali hushuka mzuka wa mistari kwa ubovu wa beat
Au anaporusha track kali dj haipigi
Mc mkali hushuka mzuka wa mistari kwa ubovu wa beat
Au anaporusha track kali dj haipigi
Juhudi za wasiojiweza



Авторы: Fareed Kubanda


Внимание! Не стесняйтесь оставлять отзывы.