Dizasta Vina - The Verteller (Intro) Lyrics

Lyrics The Verteller (Intro) - Dizasta Vina



Inafaa kunena
Inafaa kunena labda ni muhimu sijui
Labda kusimulia si karama kama wanavyosema
Ikiwa msimuliaji huingia hatarini
Labda kweli baraka ni laana njema
Wasikilizaji nasikia wana ndoto na wenyewe
Si uongo
Hadithi nzuri ndo' kilele kwa wasikilizaji
Ila ndoto ya msimuliaji
Ndoto ya msimuliaji ni kulindwa milele
Kwanini azibwe mdomo wakati ubongo unapiga kelele?
Si lazima msimuliaji apazwe la hasha!
Atandikiwe majani au aandikwe kama mwanasiasa
Lakini lengo lake awe huru msimuliaji atambe
Alindwe ili waovu waonyeswe, mashujaa watangazwe
Ona kuna wasimuliaji hukwepa pande tupu
Yani baada ya mitaji husimulia upande wa wenye nguvu
Wapo wabinafsi wanaotangaza jinsi asili ilivyowahusudu
Husimulia walivyoshinda vita wakigombea asali na wadudu
Swali ni je? Nani atasimulia hadithi ya wadudu?
Nani atasimulia kua si mara zote mchukua asali alimsulubu mdudu?
Nani atasimulia hadithi ya shetani,
Baada ya kusikia upande wa Mungu?
Baada ya kusikia upande wa Mungu
Waungwana kumbukeni ya muhimu na ziada
Kumbukeni ya uchumi jamii na siasa
Lindeni ghala la chakula na maji
Lakini msisahau kumlinda msimuliaji, ni afya
Japo kuwa msimuliaji si alama ya taifa
Lakini fikiria mtu ambaye yupo tayari kulipa gharama ya maisha
Msimuliaji hukukumbusha ulipotoka ujue unapoenda
Na hiyo ndio faida
Labda ukumbuke ya mdimu na majoka
Au simulizi za mizimu ya mloka
Au tarihi ambazo ni historia za kuziheshimu
Maana asiyeijua historia, huweza kurudia makosa
Msimuliaji hachagui upande maana hapendi kupotoka
Hafungamani na misalaba au alama za mwezi na nyota
Alama za wasimuliaji walioidondosha kheri
Waliookota sifa wakati wakiidondosha kweli
Enyi wa khaki kijani na manjano
Mmeona nyekundu ile pale?
Haijaja pale leo ipo tangu kale
Msiruhusu iwaguse
Si kwakua hamna hadhi
La hasha
Ila ile rangi anaifahamu msimuliaji
Ile rangi ni damu iliyomtoka au kumrukia
Na mchanganyiko wa pande zote za dunia
Anaijua leo, aliijua jana
Hajaisoma au kuisikia
Aliipata wakati akitafuta vya kusimulia
Na ni hivi anavyotaka kukusimulia leo
Nyakati za katikati kwenye eneo la ukanda wa kidachi
Zilizaliwa lugha tatu, Lugha ghafi
Na kati yao ilikuwepo lugha iliyoitwa lugha ya watu
Kwenye ukanda huu msimuliaji
Hakuitwa Narrator au story teller kwa kiingereza
Hakuitwa Erzahler japo kuwa ukanda huu
Ulikuwa karibu sana na Ujerumani
Hakuitwa Rawi kwakua huu ukanda haukuwa wa kiarabu
Msimuliaji aliitwa the Verteller
Kama Christopher Hitchens
Ama Professor Laurence Krauss
Ama Shaaban Robert
Ama Francis Scott Key Fitzgerald
Ama Chimamanda Ngozi
Ama Fred Saganda
Ama Alice Walker
Ama Octavia Burtler
Ama Lufufu Mkandala
Ama Rainfred Masako
Dizasta vina, mabibi na mabwana
Ni the Verteller



Writer(s): Edger Mwaipeta


Dizasta Vina - The Verteller
Album The Verteller
date of release
02-06-2021




Attention! Feel free to leave feedback.