Rorexxie feat. 20 Percent & EBL DRuCuLa - Nyumba ya milele paroles de chanson

paroles de chanson Nyumba ya milele - Rorexxie



(Mwamba La Mombala)
Wengine wananipenda, baadhi wananipoda
Wengine wananisifia, eee, wengine wananipondea
Sitoweza kuwatenga, sitoweza kuwatenga
Hata kama wakiponda daima nitawapenda
Wanaona nawabana, maovu wanayafanya
Hali hii itakuwaje mi' nitapoiaga dunia
Wengi watalia, wengine watafurahia
Siku itakapofikia utapoiaga dunia
Wengi watalia, wengine watafurahia
Siku itakapofikia mi' nitapoiaga dunia
Wali kufa-kufa nawengine kifo wananiombea
Wali kufa-kufa nawengine kifo wanakuombea
Nikifikiria kifo, kulala siwezi siitaji mpenzi na sifanyi ushenzi
Naitaji nikae tu, nimuombe mwenyezi
Siku ya kifo changu anipemema makazi
(Ukimaliza kuteseka unakwenda kule)
(Hileee ndio nyumba ya milele)
(Haina hodi, hodi, haina kodi, ileee ndio nyumba ya milele)
(Ukimaliza kuteseka unakwenda kule)
(Hileee ndio nyumba ya milele)
(Haina hodi, hodi, haina kodi, ileee ndio nyumba ya milele)
Maisha ni kutoka, kisha kuchakaa
Yani ukishafika juu nikudondoka
Umepita kwenye raha, shida ni balaa!
Pumzi imeshakata ndio unapanda moto car
Mpende mama mtenge baba ndicho umejenga
The way uta'cholipwa ndicho umetenda
Tuko up, tuko down, muda unakwenda
Tupo njia ya Kanumba na Papa Wemba
Dada, Mama, Baba m'nanitenga zikifika nitaondoka bila kupenda
Unapojenga ukipenda funga lanter nitazima kamshuma, kisha nakuenda
Naona kuna dondo kapigwa panga
Chini hakuna godoro kuna michanga
Mida yakula moto kufunga kanga
Sasa regeza kidogo, kaza kamba
Sitaki tena mbido nataka mwanga
Upepo sina majo sina nipe sanda
(Ukimaliza kuteseka unakwenda kule)
(ileee ndio nyumba ya milele)
(Haina hodi, hodi, haina kodi, ileee ndio nyumba ya milele)
(Ukimaliza kuteseka unakwenda kule)
(Hileee ndio nyumba ya milele)
(Haina hodi, hodi, haina kodi, ileee ndio nyumba ya milele)



Writer(s): Abbas 20 Percent Hamis, Abbas Hamis, Issa Rorexxie Ibungu, Issai Ibungu


Rorexxie feat. 20 Percent & EBL DRuCuLa - Brokėn
Album Brokėn
date de sortie
26-10-2023




Attention! N'hésitez pas à laisser des commentaires.