Fid Q feat. P-funk Majani - Bongo Hip Hop текст песни

Текст песни Bongo Hip Hop - Fid Q feat. P-funk Majani



Ulianza wewe, wakaja waimbaji na wabana pua
Wale mwewe, Franga wawindaji wakatusua
Kwakuwa, wanajua mshikaji unaishi kwa miko
Na zako itikadi, ziko kimziki na sio mshiko
Kama haileti hela, basi haimake sense,
No sweat kisela mie nikakomaa tu na lako penzi
Sikusound garbage au kuchange suddenly
Mie ni mjeshi so naweza fight savagely
Hiphop ya ukweli,
Ikapigwa radioni
Malaika wa kheri nao hutembelea motoni
Penzi ni kipofu na anayemuona halioni
Sikuwa na hofu, mama alinipenda tangu nikiwa tumboni
I started young, I made my mother's womb a drum
My umblirical chord a guitar, muhoji aliyenizaa
Bongo Flava mzuri kiasi, hiphop we ndo my queen
My 1st my last & everything in between
Mimi na wewe, tangu long time
Kabla ya hizi pesa kabla haijaja hii Fame
Chaajabu hujabadilika na uko Mwenye main stream
Bongo Hiphop
Bongo Hiphop
Mimi na wewe, tangu long time
Kabla ya hizi pesa kabla haijaja hii Fame
Chaajabu hujabadilika na uko Mwenye main stream
Bongo Hiphop
Bongo Hiphop
Kama kukupenda wewe ni dhambi, basi shetani yu nami
Na kamwe sintonyea kambi ili niwabambe dukani
For a million little pieces naweza kumcon Oprah ka James Frey
Na watasema sitishi wakati wanaogopa nisitokee
Waufuate mkumbo huu wa wasomi, wa midundo na mistari
Ukiwa na nyundo mkononi, ni rahisi kupigilia msumari
Sio tu bongo, mpaka Ng'ambo hakuna uhuru wa habari
Kuna uhuru wa mwenye chombo, mitambo na mwenye mali
Kujifanya hawasikii, haiwasaidii, wala haiwajengi
Unachosema ni, kamwe IPP haitompinga Mengi
Unawakumbusha wazazi wa uswazi, chati ya uteja imeingia
Na Mapusha wanauza drugs ili walishe familia
Mbaya, kuhifadhi fuvu la mtu ndani ya kabati
Mbaya zaidi ni kuwa na ndugu, halafu kichwa maji
Amka bongo lala, hiphop sio ufala, ni lazima uifate
Uaminifu ni kama mshahara, fanya kazi ili uupate
Mimi na wewe, tangu long time
Kabla ya hizi pesa kabla haijaja hii Fame
Cha ajabu haujabadilika na upo kwenye mainstream
Bongo Hiphop
Bongo Hiphop
Mimi na wewe, tangu long time
Kabla ya hizi pesa kabla haijaja hii Fame
Chaajabu hujabadilika na uko Mwenye main stream
Bongo Hiphop
Bongo Hiphop
Mapenzi ya sikuhizi, bila kugombana yanakua hayana stimu
Pia ni ruksa kushikana lakini sio kushikiana simu
Inanipa wazimu, kusikia kimwana haujaachana na Hasheem
Na bado mnawasiliana, una mpango wa kuchanganya timu?
Nakupenda hiphop, ndo maana ninarap ile mbaya
Naspit fire bila hennessy, au kula kaya
I want my art to be my legacy, kabla sijaretire,
Waanze nigwaya hawa enemies
Anyways ni hayo tu
Beef huletwa na wivu na wivu sio hiphop
MC nayetaka beef amlete Maza ake kwa strip club
Bongo flava ananipima kama nimeiva kimasomo
Anagundua mie ni dreamer pia ni believer zaidi ya Common
Cha ajabu hunitempt ili nikuache hip hop
Anaahidi atanipa good sex wewe unanipa true lover
Hajui who's next. wewe unanipa tu mashavu
Nikipaa. anaumia. anatamani nishuke chini
Nami sikutamani ustaa
Ustaa ulinitamani mimi
Nilichohitaji ni kuitumia hii sanaa ili nishee na nyinyi
Hii zawadi. niliyopewa na mpaji ninayemuamini
Mpaji aliyenivika taji ilimradi incharge ni win
Na ninaamini kuna muda huongea kwa kupitia mimi
Na hunisamehe ninapokosea. ni vyema mkanizoea nyinyi
Naweza kuona unachotaka au atakachonionyesha
Nikitoa ngoma wanaitaka wanaipata
Coz wewe ni special
Mimi na wewe, tangu long time
Kabla ya hizi pesa kabla haijaja hii Fame
Cha ajabu haujabadilika na upo kwenye mainstream
Bongo Hiphop
Bongo Hiphop
Mimi na wewe, tangu long time
Kabla ya hizi pesa kabla haijaja hii Fame
Cha ajabu haujabadilika na upo kwenye mainstream
Bongo Hiphop
Bongo Hiphop



Авторы: Fareed Kubanda


Fid Q feat. P-funk Majani - Kitaaolojia
Альбом Kitaaolojia
дата релиза
13-08-2019



Внимание! Не стесняйтесь оставлять отзывы.