Rorexxie - Mama Neema paroles de chanson

paroles de chanson Mama Neema - Rorexxie

Nikimuona Neema, na muonea huruma
Ananijua babae, hakujui mama, na
Namshukuru mungu, Neema yusalama ah
Ila ananipa machungu; "baba, wapi mama?"
Ananiuliza maswali, mengi na makali
Kila nikitafakari, huwaga mi'nakumbuka mbali
(Mama Neema Neema ulimuacha na siku nane, eh!)
(Hukuta' kungoja, ili Neema wako anyonye, ehh)
(Mama Neema Neema ulimuacha na siku nane, eh!)
(Hukuta' kungoja, ili Neema wako anyonye, ehh)
Hivi mi', ninanuksi gani, au mimi nina mkosi gani?
Au kuna kitu, kwa ndugu, jamaa, na majirani, eh?
Naogopa kusema sana, dhambi kwa maanani!
Nilizaa kamwana ikashindikana
Kama bahati bwana, nilikupata kimwana na
Nikasema na tuzae watoto, watusaidie baadae
Ulilipokea kwa furaha, ulinifuata nikukumbatie
Kumbe wewe, nakupa passport utangulie
Ilipangwa wewe utangulie mwanao abakie
(Mama Neema Neema ulimuacha na siku nane, eh!)
(Hukuta' kungoja, ili Neema wako anyonye, ehh)
(Mama Neema Neema ulimuacha na siku nane, eh!)
(Hukuta' kungoja, ili Neema wako anyonye, ehh)
Kila ninakokwenda, Neema yuko nyuma yangu mie
Na mi'siwezi kumtenga, kwani baba mie mama mie
Mara acheke mara alie, Neema mara anitanie
Naomba mollah amjalie, wazo la mama lisimjie
Najua haiwezekani, kwa kila aliye duniani
Ana miaka kumi, kila siku mama yusafarini
Na maswali ya kizushi; "mama atarudi linii-ih?"
Nayakumbuka mazishi, mi'ninabaki nauzini
Mimi nilie au ninune, hivi nini eeheh, mimi nifanyee?
(Mama Neema Neema ulimuacha na siku nane, eh!)
(Hukuta' kungoja, ili Neema wako anyonye, ehh)
(Mama Neema Neema ulimuacha na siku nane, eh!)
(Hukuta' kungoja, ili Neema wako anyonye, ehh)
20 percent, (20 Percent, 20 Percent)
Man Water, (Man Water, Man Water)
(Mama Neema Neema ulimuacha...)
(Hukuta' kungoja ili Neema...)
(Mama Neema Neema ulimuacha...)
(Hukuta' kungoja ili Neema...)

Writer(s): Abbas Hamis, Issai Ibungu

Rorexxie - Bongo Records
Album Bongo Records
date de sortie
20-12-2023

Attention! N'hésitez pas à laisser des commentaires.